Nchi 14 wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, zimeunga mkono rasimu ya azimio iliyowakilishwa na Misri kwa niaba ya Palestina, inayotaka kutupiliwa mbali azimio la Rais wa Marekani “Donald Trump”, linaloitambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israeli, huku Marekani pekee ikiipinga rasimu hiyo na kutumia kura ya veto ili kuifelisha, baada ya kugundua ya kwamba inaungwa mkono na nchi hizo.

Kwa upande wake, Dk. Riyad Al-Maliki ambae ni Waziri wa Mambo ya Nje na Wahamiaji wa Palestina, ametia mkazo kwamba kura ya pmoja ya nchi wanachama wa Baraza la Usalama, Marekani imejikuta ikibaki pekee katika suala la misingi ya sheria za kimataifa na maazimio ya jumuiya ya kimataifa.

Maliki alisema ni fursa kwa Marekani kuachana na uamuzi wake ulio kinyume cha sheria na kurudi kwenye kushikamana na Mkataba, sheria na matakwa ya kimataifa, lakini kwa masikitiko imechagua kusimama katika upande mbaya wa historia, upendeleo wa ukoloni, udhalimu na kudhoofisha juhudi zote za amani katika Mashariki ya Kati na ulimwengu mzima.

Aidha, ameitaka Marekani kufuta uamuzi wake, akitilia mkazo kwamba kutumia kura ya veto hakumlindi na majukumu yake, ambayo ni ukiukaji mpya wa misingi iliyosimamishiwa Umoja wa Mataifa, kukiuka mikataba na matendo ya taasisi zake. 

Na kwamba kura hiyo ya veto, hata kama haitobadili chochote katika hali na hadhi ya Jerusalemu kama mji mkuu wa Palestina inayokaliwa kimabavu, lakini bila shaka yoyote itabadili nafasi ya Marekani kama mpatanishi wa mchakato wa amani na mchakato mwingine wowote wa kisiasa ujao.

Maliki ameongeza kusema kuwa, kujilinda kwa nchi kupo katika kuheshimu sheria za kimataifa, sio kutoa kinga na kuwezesha Mataifa yanayokiuka na kufanya uhalifu ili kuepuka kuadhibiwa, kama ilivyo sasa na Israeli yenye utawala wa kivamizi na kimabavu.

Maliki ametia mkazo kuwa, haki ya suala la Palestina, kusimama kidete wananchi wetu na kujitolea muhanga, pia kuthibiti kwa uongozi wa Palestina katika kanuni ya kimaadili, na kuheshimu kwake misingi ya sheria za kimataifa katika kukabili uvamizi wa kikoloni na wa kimakazi, limekuwa ni suala la makubaliano ya kimataifa na kubwa zaidi kuliko kuzingatia mahesabu na masilahi madogo ya serikali hii au ile. Vilevile uingiliaji wowote katika suala hili kutoka upande wowte, ni kupunguza uaminifu wa upande huo.

Waziri wa Mambo ya Nje pia amezishukuru nchi zilizopigia kura ya ndio azimio hilo na zile nchi zilizosimama upande wa misingi yake katika haki, uadilifu na sheria za kimataifa, ambazo moja kwa moja zinaelekea katika masilahi ya taifa la Palestina na suala lake,kwa sababu Jerusalem ndio moyo ulio hai wa Palestina na ndio funguo ya amani na msingi wake.

Kwa kumalizia, Maliki ameahidi kuendeleza juhudi ili kutekeleza mpango wa uongozi wa Palestina uliomo katika hotuba ya Mheshimiwa Rais, aliyoitoa katika mkutano wa dharura ya Kiislamu katika kuilinda Jerusalem na Wananchi wetu wa Palestina, ili kufikia kukomesha uvamizi wa kimabavu na kufikia haki za msingi za Palestina, vile vile kusimamisha dola ya Palestina yenye mji mkuu wake Jerusalem, huku wakimbizi wakipalestina wakirejea nyumbani walikofukuzwa kwa nguvu,hayo yote ni kwa mujibu wa azimio namba 194.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: