Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi(CUF) Ibrahimu Lipumba amesema afya yake iko imara na hana tatizo lolote kiafya.

Ametoa kauli hiyo muda huu wakati akizungumza na Michuzi Blog kwa njia ya simu ambapo amesema anashangazwa na taarifa ambazo zipo kwenye baadhi ya mitandao kuwa anaumwa na amelazwa Hospitali ya Agha Khan.

"Nimeshangaa sana kusikia eti kuna taarifa zinadai nimepatwa na nshtuko, taarifa hizo si za kweli na ndio hizo hizo zinaitwa feck news. Nipo imara na najiandaa kwenda msikiti na baada ya hapo nitakwenda makao makuu ya chama kwa ajili ya kusimamia kikao," amesema Prof Lipumba.

Amefafanua hakuwa anajua kinachoendelea mtandaoni kuhusu yeye kwani anapoingia kwenye mtandao ni kwa ajili ya kuangalia tafiti mbalimbali na si taarifa za kuzusha.

Amesema alishangaa kuona anapigiwa simu na watu mbalimbali wakimpa pole ya ugonjwa ndipo aliposhangaa na kuanza kufuatilia chanzo cha hiyo taarifa.

Nimepata fursa ya kuzungunza kwa kirefu na prof lipumba yupo bukheri wa afya njema na ameshangazwa na uzushi kuwa ameptwa na mshutuko.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: