Mwakilishi wa QNET Tanzania, Benjamin Mariki akikabidhi vyakula kwa mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Khayraat Orphans Centre kilichopo Kigogo Kati, Bi. Khadija Hussein jana.
Mwakilishi wa QNET Tanzania, Benjamin Mariki akikabidhi mashine ya kusafishia maji ya kunywa (water purifier) kwa mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Khayraat Orphans Centre kilichopo Kigogo Kati, Bi. Khadija Hussein jana.
Na Mwandishi Wetu.

Taasisi inayojihusha na masoko ya mtandaoni QNET, imetoa msaada wa mashine yenye mfumo wa kusafisha maji (Water purifier) na chakula chenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 2 kwa kituo cha watoto yatima cha Khayraat jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutoa msaada huo, mwakilishi wa QNET Tanzania, Benjamin Mariki, alisema kuwa msada huo ni moja ya sera bora ya uwajibikaji kwa jamii ambayo inatafuta kutoa kwa jamii inayoihudumia.
Mariki alisema kuwa msaada uliotolewa kwaajili ya kituo ni pamoja na ufungaji wa mashine ya kusafishia maji, kilo 100 za Mchele, kilo 100 za maharage, kilo 100 za unga, lita 60 za mafuta ya kupikia, kilo 100 za sukari, kilo 100 za sabuni ya kufulia pamoja na biskuti, pipi na juisi.

Akipokea msaada huo, Mwasisi wa kituo cha Khayraat Orphans Centre, Bi Khadija Khussein aliishukuru kampuni ya QNET kwa kutoa msaada akisema kuwa msaada huo utawasaidia kwa kiwango kikubwa watoto walioko kituoni.

“Tunashukuru kwa msaada huo tukiwa tunatambua kuwa mashine ya kusafishia maji ya water purifier itasaidia katika kurahisisha upatikanaji wa maji safi na salama kwaajili ya watoto, hivyo kutoa uhakika wa afya kwa watoto kwa kuzuia magonjwa yanayoambukizwa kwa maji kama vile typhoid na Kipindupindu wakati vyakula vitawapa watoto nafasi ya kufurahia sikukuu ya krimasi na mwaka mpya”. Alibainisha Bi Khussein.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: