Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kabla ya ufunguzi wa Tawi jipya la Benki ya CRDB lililopo mjini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifungua rasmi Tawi la Benki ya CRDB lililopo katikati ya mjini wa Dodoma. Wengine katika picha ni Mke wake Mama Janeth Magufuli watatu kutoka (kushoto), Waziri Mkuu mstaafu Mzee John Samwel Malecela wanne kutoka kushoto pamoja na viongozi wengine wa kitaifa na wa mkoa wa Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi na Waziri Mkuu mstaafu Mzee John Samwel Malecela, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli pamoja na viongozi wengine mara baada ya kufungua rasmi Tawi hilo la Benki ya Biashara ya CRDB lililopo mjini Dodoma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amekaa na Waziri Mkuu mstaafu Mzee John Samwel Malecela, katika eneo la wateja maalum wa Benki ya CRDB ndani ya Tawi hilo jipya alilolifungua.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei mara baada ya kufungua Tawi jipya la CRDB lililopo mjini Dodoma.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiagana na baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya CRDB mara baada ya sherehe za ufunguzi wa Tawi jipya la CRDB lililopo mjini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri Mkuu mstaafu Mzee John Samwel Malecela mara baada ya ufunguzi wa Tawi la Benki ya CRDB lililopo mjini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na msanii Peter Msechu aliyekuwa akitumbuiza na Bendi yake katika sherehe za ufunguzi wa Tawi jipya la CRDB lililopo mjini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Spika wa Bunge Job Ndugai wakati alipokuwa akitoka ndani ya Tawi jipya la Benki ya CRDB lililopo mjini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea mfano wa Hundi ya kiasi cha Tsh. Milioni mia moja kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei kwa ajili ya ujenzi wa Wodi ya wagonjwa itakayojengwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt. Bilinith Mahenge hundi hiyo ya kiashi cha Tsh. Milioni mia moja (100,000,000/=) itakayotumika katika ujenzi wa Wodi ya wagonjwa itakayojengwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma. PICHA NA IKULU.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: