Tuesday, December 12, 2017

RAIS DKT. MAGUFULI ATAKA WASANII WAKAA UCHI WASHUGHULIKIWE

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli akihutubia kwenye mkutano wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi CCM mjini Dodoma. 
---
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli, ameitaka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na mamlaka nyingine husika kuwachukulia hatua kali mara moja wasanii wote ambao wanacheza wakiwa uchi kwenye video zao na kupiga picha za utupu kisha kusambaa mitandaoni.

Magufuli ameyasema hayo leo Desemba 12, 2017 wakati akihutubia kwenye mkutano wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi CCM mjini Dodoma kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu wa Jumuiya hiyo.

“Baadhi ya maadili yameanza kupotea, na nyie kama wazazi mmeshindwa kuyakemea haya. Kila unapofungulia mziki ukitaka kuwaona wanaocheza utakuta wanawake tu ndiyo wako uchi, lakini wanaume hapana, baadhi ya wanawake wanaachia viungo vyao.

“Kwa nini uwavulie hata wasiohitaji kuona uchi tena kwa wakati ambao sio muafaka? Nyinyi kama Jumuiya ya wazazi imefika wakati mnapaswa kuyakemea haya. Tunaelekea wapi sasa? Tunawafundisha nini watoto wetu? Kwani akicheza amevaa nguo hatofurahisha?

“Hata Adamu alipofanya dhambi alijiona yuko uchi, lakini hawa hawajioni wako uchi hata kama wanacheza mziki hadharani. Ifike wakati sisi kama Watanzania tuyalinde maadili yetu. Vya kukopi na kupesti tuviache. Yanayofanyika ni aibu.

“Vyombo vyetu vya habari, wasimamizi wa maadili haya wako wapi? Wizara inayosimamia haya wako wapi? Je, TCRA yenye mamlaka ya kufungia hata Televisheni inayorusha video za utupu wako wapi?” alihoji Magufuli.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu