Rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete amewataka watanzania kuwa wavumilivu kutokana na kauli zinazosemwa na vijana mitaani kuwa vyuma vimekaza wakimaanisha maisha yamekuwa magumu.

Kikwete amesema hayo leo Disemba 18, 2017 wakati akitoa salam kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu  wa tisa wa CCM ambao umefanyika Dodoma ukiendana na uchaguzi mkuu wa chama hicho.

“Hakuna kazi ngumu duniani kama urais, uzuri na ubaya wa kazi hii unakuwa mpweke, kila mmoja anakuletea shida zake wewe… Magufuli amefanikiwa kwa kiasi kikubwa ndani ya miaka miwili, inaleta matumaini kwa Taifa na kwa CCM.

“Mambo ya kufanya katika nchi ni mengi, huwezi kuyamaliza yote ndani ya miaka miwili. Tunayasikia ‘oooh mara vyuma vimekaza’, kuweni na subira, viongozi wetu ni makini, wanayatambua matatizo yanayowakabiri wananchi wetu, wanayatafutia ufumbuzi,” alisema Kikwete.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: