Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Thelesia Mmando, akimkabidhi tuzo Justino Pius aliyekuwa akisoma shule ya msingi Tusiime na kuibuka mshindi wa kwanza kitaifa na kwa Mkoa wa Dar es Salaam kwenye matokeo ya darasa la saba mwaka 2016. Tuzo hizo zilitolewa kwenye kilele cha maadhimisho ya elimu Mkoa wa Dar es Salaam jana. Wengine ni wageni mbalimbali kwenye sherehe hiyo.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Thelesia Mmando, akimkabidhi tuzo Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Tusiime ya Tabata Dar es salaam, Philbert Simon, kwa shule yake kuongoza kwa kutoa wanafunzi wengi wa kumi bora mkoa wa Dar mwaka 2016. Hiyo ilikuwa kwenye hafla ya siku ya elimu Mkoa wa Dar es salaam iliyofanyika kwenye viwanja vya sabasaba.

SHULE ya Msingi Tusiime imeng'ara kwenye maadhimisho ya siku ya elimu Dar es Salaam baada ya wanafunzi wake kumi kutunukiwa zawadi ya kuingia kumi bora kwenye matokeo ya darasa la saba mwaka jana.

Tuzo hizo zimetolewa kwenye ukumbi wa TPA Sabasaba jijini Dar es Salaam na mgeni rasmi alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Thelesia Mmando.

Mbali na wanafunzi wa shule hiyo, shule hiyo ilinyakua tuzo vyeti viwili kutambua mchango wake na mafanikio kwa kufanya vizuri kwenye matokeo ya darasa la nne na la saba. Akizungumza mara baada ya shule yake kupewa tuzo mbili, Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi na Awali Tusiime, Philbert Simon, aliushukuru Mkoa wa Dar es Salaam kwa kutambua mchango wa shule hiyo katika elimu na kuwapa tuzo.

Alisema wanafunzi wote 200 waliomaliza darasa la saba shuleni hapo mwaka huu wamechaguliwa kujiunga na shule mbalimbali hali inayowapa matumaini kuwa wanafanya vizuri.

“Ushindani hapa Dar es Salaam ni mkubwa sana lakini kwa motisha kama huu tutaendelea kufanya vizuri maana Tusiime imekuwa ikiwa ya kwanza Mkoa wa Dar es salaam kwa muda mrefu, hata leo hapa watoto wengi waliopata zawadi ni kutoka Tusiime tunashukuru sana,” alisema

Justina Pius ambaye alipewa zawadi ya cheti na ngao kwa kuongoza Mkoa wa Dar es Salaam na kitaifa kwenye matokeo ya darasa la saba mwaka 2016, alisema ataendelea kusoma kwa bidii ili kuwa daktari.

“Bidii na maarifa, usikivu darasani ni vitu ambavyo wanafunzi wanapaswa kuvipa kipaumbele maan huwezi kufaulu kwa miujiza hivyo nawashukuru pia walimu wa Tusiime maana wanafanyakazi usiku na mchana,” alisema Justina.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: