UMESHAJUA KWA NINI TUNAADHIBIWA SANA KWENYE ZEBRA?

JIBU NI SIMPO TU: Unaotuponza ni ule mtazamo wetu kuwa barabara zimetengenezwa kwaajili ya magari tu.

HUAMINI?

Wee jiulize, mara ngapi ulisimama kupisha watu kwenye zebra kama sio kwa kuzuiwa na TAA tu au ASKARI? Acha yale maeneo ya huko mikoani au vijijini barabara kuu. Hapa Dar au mijini ambako maximum speed ni 50kph?

Hujaona dereva akiwapigia honi tena ya fujo kabisa watu wanaovuka kwenye zebra? Madereva wangapi wanasima kupakia kwenye zebra? Je, hatujaona madereva wanapita na 80 au zaidi kwenye zebra, tena yenye alama ya wanafunzi wanavuka kabisa?

SIAMINI kama askari hawajui kuwa sheria inasema dereva asimame mtu anapovuka au kukaribia kuvuka ILA KILICHOPO nadhani wanataka tu kujenga UTAMADUNI wa KUHESHIMU ZEBRA kwa gharama yoyote ile.

NDIVYO ilivyo nje ya nchi, zebra zinaheshimika mno, hata gari ya polisi inasimama. Yaani kile kitendo cha dereva kuona mtu anaelekea kwenye zebra tu dereva anasimama.

SIUNGI MKONO kuonewa, ila kusemea ukweli kabisaa zebra ndio kati ya alama tunazozidharau mnoo. Hebu tuanze kubadilika kifikra. TUKUBALI TU KUWA HAWA JAMAA SASA HIVI WAMEKAZA Tuokoe hizi thelathini thelathini zetu.

Changamoto iliyopo tu ni je kwa safari za mikoani nitasimama zebra ngapi nifike saa ngapi? hasa ukichukulia sehemu nyingine zinachorwa tu kuwarihidha wananchi?

TUACHE DHARAU KWA WAENDA KWA MIGUU, TUWAPE NAFASI WAVUKE
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: