Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akimsikiliza Mkurugenzi wa Dahuu Faundation Husna Bi. Abdul alipokuwa akizungumza katika shule ya msingi Muhimbili Leo mchana wakati wa hafla kutimiza mwaka mmoja wa Taasisi ya Dahuu Faundation "Tumkumbuke Mtoto wa Kiume" inayojishughulisha na ushauri nasaha kwa malezi ya mtoto wa kiume iliyofanyika kwenye shule hiyo kulia ni Rehema Sologonhe Kaimu Afisa Elimu Wilaya ya Ilala.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akimsikiliza Bi. Rehema Sologonhe Kaimu Afisa Elimu Wilaya ya Ilala wakati wa hafla kutimiza mwaka mmoja wa Taasisi ya Dahuu Faundation "Tumkumbuke Mtoto wa Kiume" inayojishughulisha na malezi na ushauri nasaha kwa malezi ya mtoto wa kiume iliyofanyika kwenye shule hiyo kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Dahuu Faundation Husna Abdul ambaye pia amesherehekea siku yake ya kuzaliwa katika hafla hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akizungumza na wanafunzi wa shule ya Msingi ya Muhimbili wakati wa hafla ya kutimiza mwaka mmoja wa Taasisi ya Dahuu Faundation "Tumkumbuke Mtoto wa Kiume" inayojishughulisha na ushauri nasaha malezi wa malezi ya mtoto wa kiume iliyofanyika kwenye shule hiyo kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Dahuu Faundation Husna Abdul ambaye pia amesherehekea siku yake ya kuzaliwa, kulia ni Bi. Rehema Sologonhe Kaimu Afisa Elimu Wilaya ya Ilala.

Mh. Sophia Mjema amewaasa watoto wa kiume kutoficha mambo hatarishi wanayo ambiwa mara wanapokutana na mtu yeyote au ndugu yeyote wa kiume pale anapokuambia au anapokufanyia kitendo ambacho unaona si cha kawaida amesema "Msisite kuwaambia baba au mama au walezi wenu kama unaona mtu anakuambia au kutaka kukufanyia Kitendo ambacho sio cha kawaida au kukutisha kwamba usiseme nyumbani. Msifiche waambieni wazazi au walezi wenu ili kujiokoa kabla mambo hayajakuharibikia mmesikia watoto" Alisema Mkuu wa wilaya huyo.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema na Mkurugenzi wa Dahuu Faundation Husna Bi. Abdulwakicheza na wanafunzi katika hafla hiyo.
Mtangazaji wa Clouds na Mmoja wa waratibu wa Dahuu Faundation Bi Gea Habib akicheza na wanafunzi wakati wa hafla hiyo iliyofanyika kwenye shule ya Msingi ya Muhimbili.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema na Mkurugenzi wa Dahuu Faundation Husna Bi. Abdul wakipiga picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa Elimu, Wakuu wa shule za Msingi na baadhi ya watendaji wa elimu wilaya ya Ilala wakati wa hafla hiyo.
Wanafunzi wa shule ya Msingi Muhimbili wakiwa wamekaa wakifuatilia hafla hiyo.
Baadhi ya maafisa Elimu wakiwa katika hafla hiyo.
Mtangazaji wa Clouds na Mmoja wa waratibu wa Dahuu Faundation Bi Gea Habib akizungumza na wanafunzi katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye shule ya Msingi ya Muhimbili.
Mtangazaji wa Clouds na Mmoja wa waratibu wa Dahuu Faundation Bi Gea Habib akiwa na wafanyakazi wenzake katika wa hafla hiyo iliyofanyika kwenye shule ya Msingi ya Muhimbili.
Wanafunzi wa shule ya Msingi Muhimbili wakiimba katika hafla hiyo.
Wanafunzi wa shule ya msingi Muhimbili wakipita na mabango yenye ujumbe wenye ushawishi wa kumlinda mtoto wa kiume pia katika jamii.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: