Na Florah Raphael.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Mwigulu imetangaza rasmi kusimamisha zoezi la utoaji wa hati za kusafiria za jumla na kwa makundi mpaka pale watakapokuwa wameweka utaratibu wa kuendelea kufanya hivyo.

Tamko hilo limetolewa na Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Mwigulu Nchemba wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari hii leo na kusema hatua hiyo imekuja baada ya kupokea taarifa ya mateso wanayoyapata vijana wanaosafirishwa kutoka nchini Tanzania kwenda nje ya nchi kwa kisingizo cha kufanyakazi tofauti tofauti.

“Sisi kwenye Wizara yetu natoa tamko na kuelekeza kwamba nasimamisha utoaji wa hati ya kusafiri ‘Passport’ za jumla za makundi za vijana wanaokuwa wanapata mikasa hiyo ya kunyanyaswa, kutumikishwa, kuteswa kikatili na wengine kuwekwa rehani kwa masuala ya dawa za kulevya”, amesema Waziri Nchemba.

Pamoja na hayo, Waziri Nchemba amendelea kwa kusema kuwa “tunasimamisha mpaka pale tutakapokuwa tumeweka utaratibu uliyokuwa rasmi na mzuri kati ya serikali ya Tanzania na serikali ya nchi husika ambako kutakuwa na mahitaji ya aina hiyo. Mfano mzuri Kenya ilipokuwa inahitaji madaktari walitumia utaratibu uliyo rasmi kuomba madaktari hao. Kwa hiyo huo ndio utakaji wa kundi wa raia walio wengi kwa pamoja”.

Kwa upande mwingine, Waziri huyo amezitaka taasisi zote zilizopewa kibali kufanya shughuli zake nchini ziende zikafanye uhakiki wao upya kuanzia siku ya leo na kesho itakuwa mwisho na endapo hawatafanya hivyo hatua kali zitafuatwa
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: