Mmasai mmoja aliingia kwenye benki moja kule Nairobi na akaulizia mkopo kwa afisa wa mkopo aliyekutana naye pale. Akamuambia yule afisa kwamba anaenda Dubai kibiashara na atakuwa huko kwa muda wa miezi minne hivyo alihitaji kusaidiwa mkopo wa Shilingi 5,000/= za Kenya.

Afisa wa benki alimwambia kuwa benki itahitaji kitu cha kuwekwa kama dhamana (bondi) na mmasai akakabidhi funguo za gari lake mpya kabisa aina ya Mercedes Benz S class 500 lililokuwa limepaki nje ya benki.

Basi wakaandikishana pale na kusaini. Baada ya mmasai kuondoka Rais wa ile benki akabaki anacheka tu pamoja na maafisa wake kwa kile kitendo cha mmasai kuacha bondi gari lake lenye thamani ya zaidi ya milioni 50 za Kenya tena kwa kijimkopo cha Ksh 5,000 tu!

Mmoja kati ya waajiriwa wa pale benki akaliendesha lile gari kulipeleka kwenye underground garage ya benki ile kwa ajili ya kulipaki. Baada ya wiki nne mmasai akarudi, akalipa mkopo wake wa Ksh 5,000 pamoja na riba iliyokuwa na thamani ya Ksh. 150.41

Afisa wa mikopo akamwambia mmasai 'Rafiki, tumefurahi kufanya biashara nawe pia hujawa msumbufu hata kidogo kwani umeturudishia kama ulivyoahidi ila tumeshikwa na bumbuwazi kidogo... wakati umesafiri tulichunguza na kugundua kuwa wewe ni zaidi ya milionea.

Kinachotuchanganya hapa ni kwanini umechukua mkopo kiasi kidogo viile? Mmasai akajibu: "Hivi hapa Nairobi umeona kuna sehemu nyingine yeyote zaidi ya benki ambapo naweza kupaki gari yangu kwa miezi hiyo minne kwa Ksh 150.41 tu na kisha kurudi na kulikuta salama? Baada ya hilo jibu wale majamaa pale benki na Rais wao wote wakajiona viazi tu.
______________
USIMDHARAU MTU KWA MUONEKANO WAKE MASAI ALIKUBALI KUDHARAULIKA LAKIN MOYONI MWAKE ALIJUA ALIFANYALO.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: