Wednesday, January 17, 2018

MAONI YA MSOMAJI: WANAUME TUACHE UNYAMA WA KUWAUA WATOTO

Kuna vitu vinashangaza sana kwenye jamii. Bahati mbaya umegundua kwamba mtoto uliyekuwa unaamini ni wako, kumbe sio wako, umebambikiwa na mkeo. 

Sasa kumuua huyo mtoto ndio atakuwa wako akiwa kaburini? Wewe fikiria, unaitwa Jumaa Kirobwa! Una uhakika gani kama mzee Kirobwa ni baba yako halali! Si wanasema mwenye uhakika wa kujua mtoto ni wa nani ni mama! Je, kama pia wewe ulibambikwa kwa mzee Kirobwa? Tuacheni ukatili usiokuwa na mpango. 

Ukigundua mtoto si wako na bahati mbaya hutaki kumuona machoni mwako mwambie mkeo ampeleke mtoto kwa baba yake! Na ukishindwa kabisa, muache mkeo iwe kwa talaka ya kidini au hata mahakamani kwa wale wasiochana. 

Lakini kutoa roho sio suluhisho. Mtoto amezaliwa tu. Hajui lolote! Kwanza sio ajabu umebambikiwa kwa uzembe wako! Mkeo anaishi Dar es Salaam wewe upo Mwanza! Wapi na wapi? Au mwanaume upo busy na kazi 24 hrs. 

Unarudi nyumbani saa sita usiku na unaondoka saa 11 alfajiri, ukiwa hoi bin taaban kwa kuchoshwa na kazi, sasa hasira za kubambikiwa mtoto zinatoka wapi? Siungi mkono tabia za uhuni na kuzaa nje, lakini kutoa roho za watu kisa eti umebambikiwa hicho si kitu kizuri. Tuzitawale hasira zetu na si kutawaliwa na hasira..

Imeandikwa na
Kambi Mbwana.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu