Wednesday, January 10, 2018

MASAUNI ATETA NA BALOZI WA KUWAIT NCHINI

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na Balozi wa Kuwait nchini, Mohammad Alamiri(kulia) kuhusu ushirikiano baina ya nchi ya Tanzania na Kuwait katika masuala mbalimbali ya ulinzi na usalama kwa raia wa nchi hizo mbili. Mazungumzo hayo yamefanyika leo ofisi za wizara,jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Balozi wa Kuwait nchini, Mohammad Alamiri, akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni,(kushoto) kuhusu ushirikiano baina ya nchi ya Kuwait na Tanzania katika masuala mbalimbali ya ulinzi na usalama kwa raia wa nchi hizo mbili. Mazungumzo hayo yamefanyika leo ofisi za wizara,jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akipokea zawadi kwa niaba ya wizara kutoka kwa Balozi wa Kuwait nchini, Mohammad Alamiri(kulia), baada ya kumaliza mazungumzo kuhusu ushirikiano baina ya nchi za Tanzania na Kuwait katika masuala mbalimbali ya ulinzi na usalama kwa raia wa nchi hizo mbili.Mazungumzo hayo yamefanyika leo ofisi za wizara,jijini Dar es Salaam.

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu