Taifa la United Arab Emirates linaomboleza kifo cha Mama wa heshima katika Taifa hilo, Sheikha Hessa binti Muhammad Nahyan aliyefariki dunia mapema jana na kuzikwa jana hiyo hiyo mjini Abu Dhabi nchini humo.

Inaelezwa kuwa Mama huyo amejenga misikiti zaidi ya 300 barani Afrika, ukiwemo msikiti wa Kichangani uliopo Magomeni jijini Dar es salaam, nchini Tanzania, na hakuwai kuiona 'live' misikiti hiyo bali kwa kupelekewa picha tu.

Tayari taifa hilo limetangaza siku 3 za maombolezo, huku bendera zake duniani kote zikipepea nusu mlingoti, huku ikishindwa kuelezwa mara moja umri wa mama huyo.

Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi, Amen.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: