Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Ndugu Wallace Karia kwa niaba ya Shirikisho anatoa pongezi kwa mwanamichezo daktari wa Sheria Dr. Damas Ndumbaro kwa kushinda kiti cha Ubunge Jimbo la Songea Mjini.

Rais Karia amesema ushindi wa Dr. Ndumbaro unaongeza wanamichezo zaidi katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao wanaweza kuwa chachu ya maendeleo ya michezo ikiwemo mpira wa miguu.

Amesema uzoefu wa Dr. Ndumbaro katika mpira wa miguu utasaidia katika nyanja hiyo na itasaidia kupaza sauti kupitia bunge katika harakati za kushirikiana kuusogeza mbele mchezo wa soka.

“Tunaamini uwezo wa Dr. Ndumbaro katika uongozi tumemuona katika mpira wa miguu akiongoza katika sehemu mbalimbali hakika uwezo wake wa uongozi ni mkubwa na atasaidia sana kukua kwa sekta hii ya michezo, sisi TFF tunamtakia kila la kheri kwenye majukumu yake mapya na tutampa ushirikiano wote kuhakikisha tunafikia mafanikio, kwetu ni faraja kubwa kuona wana familia wa mpira wa miguu wakishinda nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo Ubunge”. Alisema Rais Karia.

Rais Karia ameongeza kuwa anaamini Dr. Ndumbaro jimbo lake la Songea Mjini litakuwa moja ya majimbo yenye mfano wa kuigwa katika maendeleo ya mpira wa miguu.

Dr. Ndumbaro amewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi kwenye mpira wa miguu na hivi karibuni Rais Karia alimteuwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya rufaa ya leseni za klabu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: