Mkuu wa mkoa Amina Masenza akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua moja ya shule ya sekondari akielekea kukagua vyoo vya shule ya sekondari ya Nyanzwa.
Mkuu wa mkoa Amina Masenza akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua moja ya shule ya sekondari na akiuliza kitu kuhusu ujenzi wa shule ya sekondari ya Nyanzwa.
Mkuu wa mkoa Amina Masenza akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua vyoo vya shule ya Nyanzwa.
Mkuu wa mkoa Amina Masenza akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua vyoo katika sekondari ya Ibumu.
Na hili ni moja ya jengo ambalo linajengwa kwa ajili ya maabara za shule ya sekondari ya Ibumu.

Na Fredy Mgunda, Kilolo.

MKUU wa mkoa wa Iringa Amina Masenza ametoa jumla ya shilingi milioni nne (4,000,000) kwa ajili ya kuchochea manendeleo ya ujenzi majengo kwenye shule nne za sekondari ikiwa na lengo la kuhakikisha kuwa wanafunzi wa shule hizo wanasoma bila kuwa na usumbufu wowote ule.

Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa shule mpya za sekondari zilizopo tarafa ya Mazombe mkuu wa mkoa Amina Masenza alisema kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dr John Pombe Magufuli imejipanga kuhakikisha wanafunzi wanasoma bila kulipia kitu mchango wowote ule utakaochangishwa na walimu.

“Mimi nimetumwa na Rais kusisimamia ila ya chama cha mapinduzi kuhakikisha inatendewa haki katika kuleta maendeleo hivyo ni lazima nihakikishe wanafunzi wanakwenda shule na sio vinginevyo maana bila wanafunzi kwenda shule Rais hawezi kunielewa nitakuwa sijatimiza malengo ya kutoa elimu bila malipo” alisema Masenza.

Masenza alisema kuwa atachangia shilingi milioni moja kwa kila shule za sekondari za tarafa hiyo ambazo zipo kwenye ujenzi na shule hizo ni Ibumu na Nyanzwa ili kuhakikisha wanafunzi wanasoma na kuwapunguzia umbali wa kutoka eneo moja kwenda eneo jingine kuifuata shule.

“Naombeni tuzikamilishe shule hizi kwa wakati ili kuwapunguzia umbali wa kusoma watoto wetu haiwezekani wanafunzi hadi kuikuta shule moja ni umbali wa zaidi ya kilometa kumi na tatu ,jamani hawa ni watoto zetu na maisha yao yanategemea elimu hivyo ni lazima tuwekeze kwenye elimu” alisema Masenza.

Masenza aliwataka viongozi wa vijiji kuhakikisha kuwa wanafunzi wote waliofulu na kuchaguliwa kuingia kidato cha kwanza wapelekwe shule kwa wakati na wazazi wote ambao hawajawapeleke shule watoto wao wachukuliwe hatua kwa kuwa Rais hataki kuskia kuwa mtoto hajaenda shule.

“Jamani Rais ameagiza kuwa wanafunzi wote wanatakiwa kuwa shule hata kama hawana sare za shule sasa huyo mzazi gani ambaye hatakiwa kuwa peleka shule naombeni kabla sijawakulia hatua nyinyi viongozi basi hakikisheni wanafunzi wote waliofaulu wanakwenda shule” alisema Masenza

Lakini mkuu wa mkoa alifanya ziara kwenye shule ya sekondari Kihesa manispaa ya Iringa na akatoa kiasi cha shilingi laki tano (500,000),shule ya sekondari Ilambilole shilingi milioni moja(1,000,000) na shule ya msingi Matembo nako alitoa kiasi cha shilingi laki tano (500,000) pesa zote hizo ni kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa majengo ya shule.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: