Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii.

Aliyekuwa kuwa mkurugenzi Mkuu Wa shirika la utangazaji nchini, Tido Muhando, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashitaka ya uhujumu uchumi.

Mhando ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi Wa Azam Media anakabiliwa na mashtaka manne ya matumizi mabaya ya madaraka na shtaka moja la kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya sh. Milioni 887.

Mhando alifikishwa mahakamani hapo nyakati za asubuhi na ilipofika saa 5:22 asubuhi aliingizwa katika ukumbi wa mahakama ya wazi kusomewa kesi yake hiyo. 
Mhando amesomewa mashtaka yake Mwendesha Mashtaka Wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai aliyekuwa akisaidiana na wakili, Aneth Mavika pamoja na Dismas Muganyizi.

Akisoma hati ya mashtaka Swai amedai, Juni 16, 2008 huko Dubai United Arab Emirates (UAE) mshtakiwa Mhando, akiwa mwajiriwa wa TBC kama Mkurugenzi Mkuu alitumia madaraka yake vibaya kwa kusaini mkataba wa makubaliano kwa ajili ya kuendesha vipindi vya utangazaji kati ya TBC na Channel 2 group Corporation ( BV1) bila ya kupitisha zabuni kinyume  na sheria ya manunuzi na kuisabishia  BV1 kupata manufaa.

Katika shtaka la pili imedaiwa, Juni 20,2008  katika eneo hill hilo, Mhando, katika utekelezaji wa kazi yake alitumia madaraka vibaya kwa kusaini makubaliano ya utangazaji wa  digital duniani kati ya TBC na BV1.

Pia imedaiwa Agosti 11,2008  na Septemba 2008 katika maeneo hayo, Mhando alisaini mkataba wa makubaliano ( kuongea wakuu wa mkataba ) kwa ununuzi, usambazajj kufunga vifaa vya usambazi na mnara wa utangazaji kati ya TBC na BVI na kuisababishia BVI kupata faida.

Katika shtaka la nne, Mhando anadaiwa, Novemba 16, 2008 akiwa Dubai ,United Arab Emirates alitumia vibaya madaraka yake kwa Kusini mkataba wa makubaliano(kuongea wakuu wa mkataba ) kwa kuendesha miundombinu ya utangazaji ( DTT broadcast infrastructure) kati ya TBC na BVI na kusababisha BVI kupata manufaa.

Katika shtaka la tano Tido anadaiwa kuwa kati ya Juni 16 na Novemba 16,2008 katika maeneo hayo ya United Arab Emirates aliisababishia hasara TBC ya Sh 887, 122,219.19.

Hata hivyo, Baada mshtakiwa Mhando amekana mashtaka hayo na yuko nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana.

Hakimu Nongwa alimtaka mshtakiwa hiyo kutoa fedha taslimu mahakamani hapo Sh 444 milioni ama hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya kiasi hicho cha fedha.

Aidha ametakiwa kuwa na wadhamini wawili ambao watasaini bondi ya milioni 500, na pia hatakiwi kutoka nje ya nchi bila ya kuwa na kibali cha mahakama.

Kesi hiyo, imeahirishwa hadi Februari 23,2018 kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali (PH). Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo umekamilika.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: