​Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Mawasiliano ya simu za Mkononi ya Tigo kanda ya Kaskazini, Henry Kinabo akizungumza wakati wa uzinduzi wa Msimu wa 16 wa Mbio za Kimataifa za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2018, Uzinduzi uliofanyika katika Hoteli ya Kibo Palace Homes mjini Moshi, Mashindano ambayo Kampuni ya Tigo inadhamini Mbio za Nusu Marathon, Km 21.
Mgeni rasmi katika Uzinduzi wa Msimu wa 16 wa Mbio za Kimataifa za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2018 ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira (Mwenye kofia) akiwa ameketi na Wawakilishi wa Kampuni zinazodhamini Mbio hizo, Tigo na TBL pamoja na viongozi wa Chama cha riadha mkoa wa Kilimanjaro, Jeshi la Polisi na Chuo Kikuu cha Ushirika -Moshi.
Mgeni rasmi katika Uzinduzi wa Msimu wa 16 wa Mbio za Kimataifa za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2018 ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira (Mwenye kofia) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa mbio hizo huku Wadhamini wa Mbio hizo Kampuni ya Tigo (Km 21) na TBL (km 42 ) wakishuhudia.​
Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Mawasiliano ya Tigo, wakijadiliana jambo wakati wa uzinduzi wa Mbio hizo ambazo hufanyika kila mwaka mjini Moshi, Mkoani Kilimanjaro.
Baadhi ya wageni waliofika wakati wa uzinduzi wa Mbio hizo ambazo hufanyika kila mwaka mjini Moshi, Mkoani Kilimanjaro.
​Mgeni rasmi katika Uzinduzi wa Msimu wa 16 wa Mbio za Kimataifa za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2018 ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira (Mwenye kofia) akiwa katika picha ya pamoja na waandaaji wa Mbio hizo pamoja na Wadhamini wakuu, Kampuni ya Tigo na TBL.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: