Wanafunzi wakiwa darasani katika hali ya Mlundikano mkubwa zaidi.
Mwl Risa Nkya akiwa darasani akiwafundisha wanafunzi wa darasa la tatu kwenye shule ya Msingi Nyankumbu iliyopo Halmashauri ya mji wa Geita huku wanafunzi wakiwa ni wengi zaidi darasani hali ambayo imepelekea wengine kukaa chini. 
Nje ya shule ya Msingi Nyankumbu baadhi ya madawati yakiwa yamebebanishwa kutokana na uhaba wa madarasa Shuleni Hapo.

Na Joel Maduka -Geita.

Afisa elimu wa shule za msingi katika Halmashauri ya mji wa Geita Bw. Yesse Kanyuma amesema Idara yake imeandikisha wanafunzi 7,713 wa Darasa la kwanza.

Bw. Kanyuma alisema malengo ni kuandikisha wanafunzi 10,109 na kwamba anaamini malengo hayo yatafikiwa kutokana na mwenendo wa uandikishaji.

“Zoezi la uandikishwaji linaendelea kwenye halmashauri yetu na hadi sasa tuna asilimia sabini na tisa (79%) hata hivyo bado tunamatarajio ya kuandikisha wanafuzi wengi zaidi kutokana na kwamba zoezi hili linaendelea hadi mwezi March”Alisema Kanyuma

Hata hivyo mtandao huu umetembelea baadhi ya shule za msingi mjini Geita na kuzungumza na Mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Nyankumbu Mwl Swalala David na Mwl Mkuu wa shule ya msingi Mbugani Florence Leonard ambao wamesema changamoto kubwa inayowakabili ni upungufu wa vyumba vya madarasa.

“Nina vyumba kumi na moja vinavyotumika lakini idadi ya wanafunzi ni zaidi ya elfu tatu na kitu ,mwaka jana nilikuwa na watoto elfu tatu na mia tano themanini na saba lakini vyumba ni hivyo hivyo aviongezeki kwa hiyo kilio kikubwa ni vyumba vya madarasa imefikia hatua tumeamua kutumia baadhi ya miradi tuliyonayo ili kujenga vyumba vitatu vya madarasa ingawa na vyenyewe havitoshi kutokana na wengi uliopo wa wanafunzi”Alisema Mwl Swalala.

Aidha Mwl. Swalala ameendelea kusema pamoja na matatizo ya uhaba wa madarasa hata hivyo bado wanakabiliwa na tatizo la madarasa kuchakaa na kutengeneza nyufa hali ambayo ni hatarishi kwa wanafunzi ambao wanasoma kwenye madarasa hayo.

“Kutokana na wingi wa wanafunzi imekuwa ni kazi ngumu sana kwa mwalimu pindi anapofundisha kumpitia kila mwanafunzi na kumuelekeza hata hivyo pamoja na changamoto hizo walimu wameendelea kujitahidi kufundisha”Alisema Mwl Leornad.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: