Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Mbarawa, akizungumza na wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Posta. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Posta, Dk. Haruni Kondo na kulia ni Kaimu Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe.
Mjumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi, Peter Bihume, Meneja wa Posta Mkoa wa Kigoma, akimuuliza swali Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa katika mkutano huo.
Mjumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi, Ahmed Kaumo, ambaye pia ni Mwenyekiti TEWUTA, akitoa neno la shukrani kwa Waziri Prof. Mbarawa.
Mkuu wa Kitengo cha uhusiano cha TPC, Elia Madulesi, akizungumza, wakati akifafanua jambo katika mkutano huo.

Kaimu Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Posta, ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, jijini Dar es Salaam leo. Wa pili kulia ni mgeni rasmi, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa.
Wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakisikiliza maelezo ya ufunguzi wa baraza hilo.
Mwenyekiti wa Bodi ya TPC, Dk. Haruni Kondo akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri Profesa Mbarawa kuufungua mkutano huo.
Baadhi ya Wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakisikiliza maelezo mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa katika ufunguzi huo.
Baadhi ya Wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akifungua mkutano huo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Mbarawa, akizungumza na wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa TPC, wakati akiufungua mkutano wa baraza hilo, jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (katikati mbele), akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa TPC, mara baada ya kuufungua mkutano huo, jijini leo. kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya TPC, Dk. Haruni Kondo na kulia kwake ni Kaimu Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: