Baba mzazi wa mtoto Samweli, Amos Hussein (39) mwenyeji wa Morogoro katikati ni Samwel Amos (2) wa kwanza kulia ni mama yake Flora Liberia (33) mwenyeji wa Kigoma ila kwa sasa wanaishi mtaa mail 35 kata ya Visiga, Halmashauri ya mji wa Kibaha mkoa wa Pwani.
Mtoto Samweli Amos miaka (2) alizaliwa Januari 3, 2013 katika zahanati ya Mlandizi iliyopo Kibaha mkoa wa Pwani, akiwa amekalishwa katika kiti walichotengeneza wazazi  kwaajili ya kumketisha mtoto huyo kama inavyoonekana hapo.

Na Vero Ignatus Pwani.

Mkazi wa eneo la Maili 35,  Kata ya Visiga katika Halmashauri ya Kibaha Mjini Bi Flora Liberia (30) ameelezea masikitiko yake kutokana na kutaabika na ulezi wa mtoto wake Amos Samwel mwenye umri wa miaka miwili na nusu ambaye tangu alipozaliwa viungo vyake havijakaza hali iliyosababisha kushindwa kufanya shughuli zake za kujiongezea kipato.

Bi. Flora ambaye ni mama wa nyumbani anaomba kupatiwa msaada ili aweze kumtibu mwanae ambae amekuwa akitaabika kwa muda mrefu sasa ili aweze kuokoa maisha yake.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: