Mkurugenzi wa masomo Airtel Tanzania Isack Nchunda akiongea Jijini Dar es Salaam leo wakati wa gawio kwa wateja na mawakala wa Airtel money ambapo jumla Sh bilioni 1.7 zitatolewa kwa robo ya mwaka iliyoisha Disemba 2017.kushoto ni Meneja huduma za Airtel money Ibrahim Malando na Meneja uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando.
Meneja huduma za Airtel money Ibrahim Malando akiongea Jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutangaza gawio kwa wateja na mawakala wa Airtel money ambapo jumla y sh bilioni 1.7 zitatilewa kwa robo ya mwaka iliyoisha Disemba 2017 katika ni Mkurugenzi wa masoko Airtel money Tanzania Isack Nchunda na Meneja uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando.

Na Agness Francis, Globu ya Jamii

KAMPUNI ya simu za mkononi Airtel imetangaza rasmi kugawa gawio la Sh.bilioni 1.7 kwa kila robo ya mwaka kwa wateja wake wote wanaotumia Airtel Money ikiwa ni mara ya tano kufanyika tangu ianzishwe huduma hiyo mwaka 2015.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Masomo Airtel Money Isack Nchunda, amesema kuwa leo wametoa rasmi Sh, bilioni 1.7 ambayo ni riba ya robo ya mwaka iliyopita ikiwa zoezi hilo litakuwa endelevu badala ya ule utaratibu wa mwanzowa kila miezi sita ambapo gawio hilo la faida litawafikia moja kwa moja walengwa ambao ni wateja pamoja na mawakala wote wanaotumia huduma hiyo ya Airtel Money hapa nchini.

Amefafanua Nchunda amesema Mr. Money atarudisha gawio kulingana na salio linalosalia katika akaunti kila siku kwa anayetumia huduma hiyo ambayo mteja atakuwa huru kufanya matumizi yake binafsi kama kununua bando, luku, na mahitaji mengine kupitia riba hiyo bila kupangiwa na Mr. Money huyo.

Kwa upande wake Meneja wa Huduma za Airtel Money Ibrahim Malando, amewataka mawakala hao kuendelea kufanya huduma bora kwa wateja wao kwani ni hatua nzuri ya kujiongezea zaidi faida kwa gawio lijalo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: