Baadhi ya watoto wa Makao ya Taifa ya Watoto wakiimba mbele ya wageni kutoka wafadhili wa Makao yao Abbot Tanzania pamoja na uongozi wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto jijini Dar es Salaam.
Baaadhi ya Maafisa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na Wafanyakazi wa Makao ya Watoto wakifuatilia kwa makini maigizo ya Watoto wanalelewa kituoni hapo pichani ni Bi. Ferediana Kiromo kushoto na kulia kwake ni Beatrice Mwatujobe wote kutoka Wazira ya Afya.
Mlezi wa Makao ya Taifa ya Watoto Bi. Beatrice Mugubilo akiongoza wageni wa Makao yake kuangalia maendeleo ya miradi inayofadhiliwa na Mfuko wa Abbot Tanzania.

Na Anthony Ishengoma.

Watoto wanaoishi katika Makao ya Taifa ya Watoto Kurasini wamefaidika na huduma ya Bima ya Afya kwa ajili ya matibabu yao baada ya shirika la Abbot Tanzania kuwezesha ufadhili wa huduma hiyo muhimu pamoja kuwafungulia akaunti za benki ili waweze kumudu kulipia upya wakati bima zao zinapofikia mwisho wa muda wake.

Shirika hili limekuwa mfadhili mkuu wa Makao ya Taifa ya watoto tangu mwaka 2001na limewezasha watoto wa kituo hiki kuhakikisha wanapata huduma mbalimbali ikiwemo ustawi wa watoto kiafya na huduma nyinginezo kama vyeti vya kuzaliwa, ujenzi wa mabweni pamoja na huduma za miundombinu ya kituo hicho.

Makao ya Taifa ya watoto wenye shida Kurasini yametembelewa na ujumbe maalum katoka Shirika linalofadhili kituo hiki la Abbot Tanzania ili kujionea Maendeleo ya shughuli za kituo hicho zinazofadhiliwa na shirika hilo.

Akiongea wakati wa kuwakaribisha wageni hao kituoni hapo, Kaimu Kamishina wa Ustawi wa Jamii Simon Panga amesema Shirika la Abbot Tanzania limekuwa likitoa ifadhili wake kwa kituo hiki tangu mwaka 2001 na kufanikiwa kuleta mageuzi makubwa kwa Maendeleo ya kituo hiki.

Kamishina Panga ameongeza kuwa pamoja na ufadhili was shirika la Abbot Tanzania, serikali imehakikisha huduma muhimu kama vile chakula, malazi, mavazi, matibabu na elimu vinapatikana kwa watoto wote wanaoishi katika Makao ya Watoto Kulasini.

“Watoto huletwa katika kituo hiki kupitia Maofisa wa Ustawi wa Jamii kutoka Hamashauri zote nchini wakiwa na taarifa zilizokamilika kulingana na mazingira waliyotoka na kuanza maisha kituoni hapa kwa ufadhili wa wasamalia na wafadhili kwa kushirikiana na serikali amesema Kamishina Panga.,”

Historia ya kituo inaanza mwaka 1966 pale Wamissionari walipokianzisha kwa lengo la kulea Watoto yatima. Kituo kilianza na idadi ya Watoto watatu na baadaye kukabidhiwa rasmi kwa serikali ya Tanzania mwaka 1968 na tangu wakati huo serikali ilibadili mfumo wake na kuanza kutoa huduma ya malezi kwa watoto wote wenye shida.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: