Mbunge wa njimbo la Mufindi kaskazini Mahamuod Mgimwa akiwakabidhi zawadi ya mbuzi kwa walimu wa shule za msingi waliofanya vizuri katika moja ya kata iliyopo jimboni kwake.

Na Fredy Mgunda, Iringa

Wananchi wa jimbo la Mufindi kaskazini wametakiwa kuwapeleka watoto wao shule kwa lazima kwa kuwa elimu inatolewa bure na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Mafuli kwa lengo la kuhakikisha kila mwanafunzi wote waweze kupata elimu na kuondoa ujinga na kuleta maendeleo kwa taifa.

Hayo yamesemwa na mbunge wa jimbo la Mufindi kaskazini Mahamuod Mgimwa alipokuwa kwenye ziara ya kukagua miundombinu ya shule zilizopo katika jimbo hilo ili kuweza kuzitatua changamoto zilizopo katika maendeo hayo.

Akiwa bado yupo kwenye ziara hiyo mbunge huyo aligundua kuwa wazazi wengi wamekuwa kikwanzo cha kuwapeleka shule watoto wa hivyo akawataka viongozi wote wa serikali za vijiji kuwa chukulia hatua wazazi ambao hawatawapekeka shule watoto wao.

Mgimwa alisema kuwa yupo tayari kunyimwa kura na wananchi ambao atawachukulia hatua za kisheria kwa kutowapeleka shule watoto wao kwa ajili ya faida ya maisha yao.

“Nasema kweli nitakubali kuachia ngazi ya kuwa mbunge kwa kunyimwa kura za wananchi wasiopenda maendeleo ya watoto wao,hadi sasa shule zimefungua lakini wazazi hawawapeleki shule watoto nitahakikisha wanachukuliwa hatua za kisheria” alisema Mgimwa

Aidha Mgimwa alisema kuwa sasa imefika mwisho kwa watoto wa jimbo la Mufindi Kaskazini kuwa soko la wafanyakazi wa kazi za ndani wakati wanauwezo wa kuwa viongozi hapo baadae.

“Nasema tena haiwezekani kila mfanyakazi ukifika daresalaam utasikia katoka Iringa jimbo la Mufindi Kaskazini sasa sitaki kusika swala hilo na wazazi wanaofanya hivyo nitawachulia hatua za kisheria serikali ya awamu ya tano inataka kuwa na wasomi wengi ili kuasaidia maendeleo ya nchi”alisema Mgimwa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: