Meneja Mkuu wa Migodi wa Bulyanhulu Benedict Busunzu akikabidhi hundi ya milioni 75,649,524 kwa Mkuu wa wilaya ya Nyangh’hwale Hamim Gweyama kwa ajili ya malipo ya ushuru wa huduma kwa halmashauri ya wilaya ya hiyo katika kipindi cha mwezi Julai hadi Disemba 2017.
Meneja Mkuu wa Migodi wa Bulyanhulu Benedict Busunzu akizungumza na madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale ambapo alisema Acacia itaendelea kushirikiana na serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi .
Meneja Mkuu wa Migodi wa Bulyanhulu Benedict Busunzu akifurahia pamoja na wafanyakazi wa Bulyanhulu baada ya kukabidhi hundi kwa halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale.
Na Joel Maduka, Nyang'hwale.

Kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu Acacia kupitia mgodi wake wa Bulyanhulu imekabidhi hundi ya shilingi milioni 75,649,524 kwa halmashauri ya wilaya ya Nyang’hwale Mkoani Geita kwa ajili ya malipo ya ushuru wa huduma kwa kipindi cha Mwezi Julai hadi Disemba mwaka 2017.

Akikabidhi mfano wa hundi hiyo mbele ya madiwani wa halmashauri hiyo Meneja wa Mgodi huo, Benedict Busunzu, alisema kawaida mgodi huo hutoa ushuru kwa Wilaya mbili ya Msalala na Nyangh’hwale kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Aidha alitaja moja ya miradi mingine ambayo mgodi huo umesaidia Wilayani humo ni pamoja na mradi wa mkubwa wa kusambaza maji kwa wakazi 150,000 wilayani humo, wenye gharama ya Shilingi Bilioni 4.5 ambao unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.

Aidha kwa upande wake Katibu tawala wa Mkoa wa Geita, Celestine Gesimba amewataka madiwani na watendaji wa halmashauri ya hiyo kuepuka kutumia fedha zinazotolewa na wadau mbali mbali kwa ajili ya miradi ya maendeleo kwa kulipana posho za vikao, badala yake zote zitumike katika miradi kwa manufaa ya ustawi wa wakazi wa Wilaya hiyo.

“Ninapenda kuwaonya viongozi na watendaji ambao mpo hapa Nyangh’wale kuwa tusitumie hizi fedha kwa ajili ya kulipana posho za vikao badala yake zote zietumike katika miradi ya maendeleo kwa jinsi mtakavyoainisha,”alisema Gesimba.

Aidha Mkurugenzi wa Wilaya ya hiyo, Carlos Gwamagobe, pamoja na kushukuru mgodi mgodi huo kwa kuwapatia fedha hizo alisema ushuru wa huduma ambayo walikuwa wakipata hapo awali umeshuka kwani kwa kiasi kikubwa kwani walikuwa wakipokea milioni mia nne kwa miezi sita .

“Tuna imani kuwa mgodi huu ukianza shughuli zake kama ilivyokuwa awali hata ushuru wa huduma utaongezeka kwani awali tulikuwa tukipatiwa kiasi cha Shilingi Milioni 225 lakini tangu kuibuka kwa sakata la Makinikia, ushuru nao umepungua mara mbili ya zile za awali,”alisema Gwamagobe.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: