Dkt Godwin Mollel akikabidhiwa cheti cha uthibitisho kwa kuchaguliwa kwake na Msimamizi wa Uchaguzi katika jimbo hilo Valerian Juwal
Dkt Godwin Mollel akifurahia pamoja na watu aliombatana kushuhutia tukio hilo
Na Dixon Busagaga, Siha

Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia mgombea wake Dkt Godwin Mollel kimeshinda kiti cha ubunge katika jimbo la Siha baada ya kupata kura 25,611 sawa na asilimia 80 akimshinda mpinzani wake Elvis Mosi (Chadema) aliyepata kura 5,905 sawa na asilimia 18.5.

Akizungumza kabla ya kukabidhi Cheti cha uthibitisho kwa kuchaguliwa kwake,Msimamizi wa Uchaguzi katika jimbo hilo Valerian Juwal amesema mgombea Tumsifueli Mwanry (CUF) amepata kura 274 sawa na asilimia 0.9 huku mgombea wake chama cha Sauti ya Umma (SAU) akipata kura 170 sawa na asilimia 0.6.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: