Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo, imeiahirisha kesi ya uhujumu uchumi inayomkabiki mmiliki wa IPTL, Harbinder Singh Sethi na mfanyabiashara James Rugemarila hadi Machi 2, mwaka huu.

Hatua hiyo imekuja baada ya Mwendesha Mashtaka kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Leornad Swai kudai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shahidi wakili Swai ameomba kesi hiyo iahirishwe kwa kuwa bado wanafuatilia hatua ya upelelezi.

Kutokana na taarifa hiyo, Wakili wa utetezi, Michael Ngalo aliiomba Mahakama waelezwe upelelezi umefikia wapi ili wajue kipi kinaendelea.

Hata hivyo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi, ameiomba Mahakama kutoruhusu suala la ugonjwa wa washtakiwa kuwa linasesemwa semwa mahakamani hapo kwa kuwa hilo ni suala la kitaaluma zaidi, (Kitabibu).

Amedai, masuala ya ugonjwa ni la mtu binafsi linapaswa kujadiliwa nje ya Mahakama isipokuwa pale tu Mahakama inapotakiwa kutoa amri na si vinginevyo.

"Mahakamani hapa si mahali sahihi sana pa kuleta masuala ya ugonjwa, kwanza watakuwa hawawatendei haki wateja wao,amedai Kishenyi kutokana upande wa mashtaka mara kwa mara kesi hiyo inapokuja kwa ajili ya kutajwa kuwa wanalalamikia afya za wateja wao.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 2, mwaka huu. Kwa pamoja washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi, utakatisha fedha na kuisababisha Serikali hasara ya USD 22, 198,544.60 na Sh.Bil 309.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: