Wednesday, February 28, 2018

MAMA AMCHINJA MWANAE NA KUMFICHA UVUNGUNI


Na Dixon Busagaga wa MMG -Kilimanjaro.

JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Hadija Msangi (30 ) mkazi wa Mwanzini kwa tuhuma za kumchinja mtoto wake mwenye umri wa miezi tisa na kitu chenye ncha kali shingoni hadi kufa .

Mtoto aliyeuawa ametambulika kwa jina la Hashim Msuya na kwamba mtuhumiwa baada ya kufanya unyama huo aliuweka mwili wa mtoto huyo kwenye mfuko wa Safleti na kuuhifadhi kwenye uvungu wa kitanda chake.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi wa Polisi , Hamis Issah amethibitisha kutokea kwa tukio hilo mnamo Februari 26 mwaka huu majia ya saa 10:00 katika kata ya Msangeni wilaya ya Mwanga na kwamba tayari uchunguzi wa kidaktari umefanyika.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu