Kila jambo hakika huwa halikosi mwisho msemo huu huwa na ukweli ndani yake ilikuwa kama ndoto kwa Mama wa mitindo Asya Idarous Khamsin kutangaza kuandaa jukwaa la Lady in Red, lakini ndoto hiyo imetimia kabisa bila kipingamizi mbele ya hadhara kubwa ya watu usiku wa 9 Feb 2018 ndani ya King Solomon Hall.

Lady in Red 2018 limekuwa ni Onyesho la Mwisho kwa Designer mkongwe ambaye ndiye mwanzilishi wa Onyesho hilo Asya Idarous Khamsin. Kiukweli Jukwaa la mwisho la Lady in Red lilikuwa na mvuto, kwa taswira ya mbali inaonyesha kabisha ni jukwaa ambalo lilikuwa na ushirikiano mkubwa sana wa wadau na wanamitindo wengine tofauti ilivyo zoeleka.

Mwisho ni pongenzi kwa Asya kwa kuamua kuwaachia jukwaa wanae yaani Designers walio lelewa na Lady in Red, maana angekuwa na roho mbaya pengine Onyesho lingeishia mitini Hongera sana Asya.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: