Mkurugenzi wa Msama Promotions Ltd, Alex Msama akizungumza na Waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na maandalizi ya tamasha la pasaka linalotarajiwa kurindima Kanda ya Ziwa.
Waimbaji wa nyimbo za Kiroho (Injili), Afrika Mashariki na Kati Christina Shusho na Solomon Mukubwa wanatarajiwa kuwaburudisha kiroho vilivyo,watakapokuwa wakitumbuiza katika jukwaa la Tamasha la Pasaka 2018,ambalo safari hii linafanyika Kanda ya Ziwa, mkoa wa Mwanza na Simiyu.

Akiwatangazia Mashabiki wa Tamasha la Pasaka jijini Dar Es Salaam hapo jana,Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw, Alex Msama alisema kuwa mbali ya uzinduzi wa Mwimbaji Nyota wa nyimbo za Injili,Rose Muhando pia waimbaji hao wamethibitisha kuzindua na kuzitangaza nyimbo zao mpya.

Msama amesema kuwa Waimbaji hao wana nyimbo nzuri na zenye kumuimbia,kumsifu na kumtukuza Mungu,nyimbo ambazo anaamini zitavuta hisia za wengi watakapozikia.

"Solomoni Mukubwa na Shusho wote hawa hawajasikika muda mrefu katika majukwaa,hivyo wakazi wa Kanda ya Ziwa wakae mkao wa kuzifurahisha roho na wajitokeze kwa wingi katika maonesho hayo yatakayofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Aprili 1 na Uwanja wa Halmashauri mjini Bariadi mkoani Simiyu Aprili 2 mwaka huu",alisema Msama.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: