Katika michakato ya kukusanya taarifa zaidi kuhusu usalama wa wanamuziki kazini, nimekutana na mzee mmoja kanihadithia kuwa siku moja miaka ya 1960 huko Kiko Kids walikuja Dar es Salaam, yeye na rafiki zake walitembea kwa mguu toka Magomeni mpaka Kariakoo kuifwata bendi.

Muziki ulipoisha wakapata woga kuvuka Jangwani usiku, wakaenda kituo cha polisi na kuomba kusindikizwa. Polisi akapatikana akawasindikiza mpaka mlangoni kwa nyumba zao. Safari ya mguu toka Kariakoo mpaka Magomeni. Baada ya kuhakikisha wamefika salama polisi akarudi Kariakoo.

SWALI HIVI LEO UKIENDA KITUO CHA POLISI KUOMBA KUSINDIKIZWA KWENU ITAKUWAJE? HEBU TUTIRIRIKE...

Na Anko Kitime.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: