Picha: Gazeti la Daily monitor la leo Feb 9, 2018 la Uganda kuhusu matokeo ya kidato cha nne.

Kumekuwa na mjadala mzito katika Bunge la Uganda na pia mitaani kuhusu matokeo ya kidato cha nne yaliyotangazwa jana mchana huku takribani wanafunzi wengi wamefutiwa matokeo.

Huku mtaani kumekuwa na mawazo tofauti huku wengine wakihoji je hao wanaotaka Waziri husika ang'atuke wao wanapata wapi uhalali wa kuhoji ilihali matokeo yao walio wengi pia yalifutwa wakati wa chaguzi na kurudiwa?

Katika haya yote mimi swali linalonirudia ni je chanzo cha tatizo ndicho kinachozungumziwa (Tanzania / Uganda) au tunazunguka mbuyu?

-Je wazazi wanatimiza ulio wajibu wao?
-Je jamii (mimi na wewe) inatimiza wajibu wake?
-Je wanafunzi wanatimiza wajibu wao?
-Je walimu wanatimiza wajibu wao?
-Je Serikali ifanye nini ili kuinua ufaulu?

Nitashukuru ikiwa kuna mtu ana maoni juu ya namna anavyotazama tatizo la elimu na njia zinazoweza kutumika kukwamua mkwamo ambao unazungumzwa hapa na pale.

MUNGU akubariki
Asante.
Godwin Msingwa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: