Pichani ni moja ya kituo cha kupigia kura zilizifanyika Jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Jana Februari 16, 2018 nilimsikia Mkurugenzi wa uchaguzi ndugu Ramadhani Kailima akiwaonya kituo cha ITV na kusema atawachukulia hatua kwa hatua yao ya kumuhoji msimamizi wa uchaguzi ndani ya kituo cha kupigia kura na baadae nikawasikia ITV wakiomba radhi.

Kwanza niwapongeze sana ITV, chombo hiki kimekuwa mahiri sana wakati wa uchaguzi,nathubutu kusema kuwa ITV wamekuwa namba moja kila wakati linapokuja suala la uchaguzi, kidogo niliona Azam waliwatikisa wakati wa uchaguzi mkuu wa 2015.

ITV walifanya kile ambacho watazamaji wa TV Tanzania wanakihitaji,haiwezekani nchi ipo kwenye joto la uchaguzi, wewe chombo chako kinapiga muziki ama kianendelea na maigizo,huko ni kuinajisi taaluma! hongereni sana ITV.

Sasa nije kwa hili la Kailima la kuwaonya ITV!

Kwanza umekuwa bi utaratibu tangu 1992, linapofika suala la uchaguzi waandishi huweka kambi kwenye vituo vya uchaguzi!.

Kwenye uandishi kuna kitu kinaitwa "Checklist" huu ni mwongozo wa nini kinatakiwa kwenye story, mfano kwenye stori ya soka, checklist inataka utuambie...

1. Matokeo

2. Majina ya timu

3. Wachezaji waliofunga

4. Idadi ya kona,adhabu,umilikinwa mpira,mashuti yaliyopigwa langoni na kulenga na yale ambayo hayakulenga goli.

5. Jezi za timu

6. Maoni ya makocha,wachezaji na mashabiki pamoja na wataalamu.n.k.

Linapokuja suala la uchaguzi, watazamaji, wasomaji, wasikilizaji hutarajiwa mwandishi awape

1. Majina ya vyama na wagombea

2. Idadi ya wapiga kura

3. Idadi ya vituo

4. Mshindi na kura alizopata

5. Mwenendo wa uchaguzi mfano vifaa vya zoezi la kupigia kura,je vilifika kwa wakati?vilitosha?vilikuwa salama?

6. Maoni ya wagombea na viongozi wa vyama juu ya mwenendo mzima wa uchaguzi mpaka baada ya matokeo

7. Maoni ya maafisa wa uchaguzi,wasimamizi wa uchaguzi n.k

8. Maoni ya maafisa wa jeshi la polisi (RPC) linapokuja suala la usalama.

9. Maoni ya waangalizi wa uchaguzi.

Haya yamekuwa yanafanyika miaka yote na hakuna aliyeonywa wala kuadhibiwa,haya ni matakwa ya wasikilizaji na watazamaji!.

Tume wametunga sheria yao ya kuwathibiti waandishi na siku hizi naona eti hata suala lankuripoti uchaguzi ni mpaka upewe ruhusa,tena unakuta tume inaamia mpaka idadi ya waandishi kutoka kwenye chombo cha habari!.

Nadhani hii si sawa, bunge libadili sheria hii, kinachohikizwa hapa siyo uandishi wa habari bali ni matangazo tu kuhusu uchaguzi.

Uandishi wa habari hujikita zaidi kuibua yale yaliyojifika na siyo yanayojulikana,uandishi wa habari ni kuandika yake ambayo wengine hawataki yajulikane!.

Kama ITV wataadhibiwa hili litakuwa pigo kwenye tasnia ya habari, uandishi wa habari za uchunguzi huenda mpaka nje ya sheria na kanuni zinasema nini?

Lengo kuu ni kuibua yaliyojificha kwa mgongo wa sheria na kanuni,ITV jana hawakutakiwa kuishia kuripoti 5W +H, walitakiwa waje na habari mpya ambazo sisi ambao hatukuwa field hatuyajui.

ITV walitakiwa kwenda mbali na kufanya habari za uchaguzi,kuibua yale yaliyonyuma ya uchaguzi huo,ambayo wengine wasingependa yajulikane!

Na ndicho walichokifanya ITV, Mkurugenzi wa Tume alitakiwa aseme walichosema ITV kilikuwa uongo ama ukweli kuhusu sanduku kinalodaiwa kupotea!

ITV walimhoji mtu akadai kuna sanduku limepotea, ITV waliona ni halali kubalance tuhuma wakamhoji afisa wa tume aliyekuwa ndani ili kuondoa ukakasi! natukumbuke walikuwa live! ITV walitakiwa kupongezwa kwani waliona hatari ya kurusha habari ya upande mmoja na yalikuwa matangazo ya moja kwa moja.

Hapa ITV walikuwa weledi, waliona umuhimu wa kubalance, stori ile ilihamia kwenye uchunguzi, tuhuma za kupoteza boksi ni story kubwa kwa ITV na chombo chochote, huwezi izima storI kubwa kama hiyo!

Poleni ITV kwa kuonywa kwa hiki kinachoitwa kukiuka sheria, ila hongereni jana mlionesha jinsi mlivyo mahiri!.

NI MIMI ABDULAZIZ AHMEID.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: