Naitwa Mzee Philip Bernard Mlay Namshukuru Mungu kwa hii Miaka 72 aliyonipa kuishi na Kuona Mengi, nakaaa Kijitonyama na pia nina maeneo kule Salasala jijini Dar es Salaam.

Nimeona mijadala Mingi ikisema Mhe Paul Makonda Hana Mamlaka ya Kusimamisha Utendaji kazi wa Mabaraza ya KATA ,baadhi wanasema Amefanya Jambo jema lakini Hakuwa na Mamlaka Nianze kwa wenye Mamlaka wamefanya nini wakati Changamoto ya Dhuluma katika Haya Mabaraza ya Kata zinanongezeka kila siku? Kwani wenye Mamlaka Hawajui au kuona?, Leo Tanzania kilio kikubwa ni Mabaraza ya Kata kutumika ISIVYO , watu wanaumia na kuteseka na wenye Mamlaka wapo, Nyumba zimeuzwa, watu wamekuwa MASKINI , yatima wanateseka, wajane wanalia kwa Kuporwa Nyumba na Ardhi , Hivi mlitaka Makonda nae aingie kwenye Mkumbo wa kuendelea kukumbatia UFEDHULI huu? Mlitaka apeleke Muswada Bungeni wa Kuondoa au kurekebisha kasoro hizo? Kwani Makonda ana Mamlaka hayo na UKU ?

Kama HUJUI , basi Tambua kuwa katika Mkoa wa Dar es Salaam Hakuna Kipande cha Ardhi chenye Thamani ya Milioni Tatu na kama Kipo utakuwa UCHOCHORO au Open Space , kwa mtazamo huu Sheria na Kanuni na taratibu zilizoanzisha Mabaraza ya Ardhi ya Kata kwa Mkoa wa Dar es Salaam HAYAPO , na kama yapo HAYATAKIWI KUFANYA KAZI KWA MUJIBU WA SHERIA ya Ward Tribunal Act, 1985 . mana yamepewa mamlaka ya kusikiliza Mashauri yasiyozidi Gharama ya Milioni 3 TU , lakini Leo utaona yanasikiliza kesi na Kubomoa Nyumba zilizojengwa kwa thamani .
Ndugu zangu Kwa Mujibu wa Sheria iliyoanzisha Haya Mabaraza inasema hayaruhusu Mtu Mwenye Taaluma ya sheria au mwanasheria kuwa mjumbe au Kiongozi, sasa yanakwenda kusikiliza nini wakati Mikataba ya Ununuzi wa Viwanja, mashamba au makubaliano ya Ununuzi na uuzwaji wa Ardhi yanafanywa kwa Wanasheria kwanza, sasa hawa wajumbe wanasemaje mikataba iloyoandikwa KISHERIA wakati wao hawajui Sheria? Wanatatua nini? Ni sawa na Ngoma ya Mdundiko umlete Mchaga hata akisikiliza Mdundo hawezi Zungusha Nyonga .

Nimefanya utafiti Kidogo katika baadhi ya Mahakama za Wilaya mashauri Karibu asilimia 90 yanatoka Mabaraza ya Kata sasa mnataka Makonda nae aendelee kujaza Mashauri Kwenye mahakama za Wilaya?

Kwenu Nyinyi mnaosema Makonda Hana Mamlaka ya Kusimamisha kazi za haya Mabaraza ya Kata, Naomba mkasome The Regional Administration Act, 1997 Section 5(1) and (3) provides; "The Regional Commissioner shall, be the principal representative of the Government within the area of the region for which he is appointed and for that purpose all the executive functions of Government in relation to that region shall be exercised by or through the Regional Commissioner"

Kumbukeni Haya Mabaraza ya Kata sio Mahakama , na Haya mahusiano yoyote na Mahakama hivyo mnaosema Makonda ameanza Kugongana na Mihimili mingine mnazidi KUKOSEA

Ukishasoma hiyo Naomba utafakari Nami hapa kitu hiki, ingekuwaje kama watu zaidi ya Elfu tatu na zaidi waliokusanyika ofisini kwa Mhe Makonda wakati wa zoezi la kuwasikiliza Matatizo yao au pale Dimond jubilee jana wangeamua kuchoma moto au kupiga Wafanyakazi wa Manispaa wanaohusika na masuala ya Ardhi Leo situngekuwa tuko kwenye MACHAFUKO makubwa ya umwagaji DAMU mana watu wakidhulumiwa na kuchoka huamua kuchukua Sheria mkononi, Kwahiyo tulitaka tuyaone Haya wakati Makonda ni Mkuu wa Kamati ya Ulinzi na usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam, Makonda yuko SAHIHI kimamlaka kusitisha kazi za Haya Mabaraza ya Kata mana yalikuwa yanahatarisha AMANI na usalama wa eneo lake la KIUTAWALA .

MWISHO , nimebaini idadi kubwa ya watu wanaompinga Makonda katika Hili ni Wale Matajiri " UCHWARA " wanaotumia vijisenti vyao kudhulumu Haki za MASKINI na hawa wako wachache sana ila wanaodhulumiwa ni WENGI , pili wasiopenda hii hatua ya Makonda ni baadhi ya Wanasiasa Njaa ambao kwao hata Mabomba ya Maji yakipata Neema yakutoa Asali na Maziwa wataendelea kukutukana tu kwao wanatumia SIASA katika kila jambo zuri na la heri kwa nchi, hawa wana CHUKI , HILA NA ROHO MBAYA TU kwa kuwa Mhe Rais, Dkt. John Pombe Magufuli na wasaidizi wake wakiwemo Kina Makonda na wengine wanaipeleka Nchi katika Mwelekeo SAHIHI uliokuwa ukisubiriwa kwa Miaka Mingi.

Mhe Paul Makonda (MWAMBA) Endelea na MASKINI wako, Endelea kuwasaidia wana Changamoto Nyingi sana ambazo ukizishughulikia kwa dhati hutapata hata dakika moja ya kuwajibu watu wa ajabu ajabu.

Kumbukeni Yesu Kristo wakati anaendelea na kazi zake za kuponya na kufufua wafu, baadhi ya Wayahudi walimuuzi Unapata wapi Mamlaka ya kufanya yote Haya nadhani kwa wa Kristo mnajua majibu ya Yesu alichowajibu baadhi ya Wayahudi

Nawatakia Jumapili Njema
Mzee Philip Bernad Mlay wa kijitonyama na Salasala
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: