Marehemu Kingunge enzi za uhai wake.
Kingunge na Peres enzi za ujana wao.

KUFUATIA kifo cha mwanasiasa mkongwe, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru aliyefariki dunia usiku wa kuamkia Februari 2, 2018 katika Hospitali ya taifa Muhimbili, picha za ujana za mzee huyo na mkewe Mama Peras Kingunge zilizotolewa na familia zinaonesha jinsi gani wakongwe hawa walikuwa na mapenzi ya dhati na kuvumiliana tangu ujana wao mpaka umauti unawafika.

Aliwahi kuwa mtumishi wa umma kwa zaidi ya miaka 50 ikiwa ni mwezi mmoja tangu mkewe Mama Peras Kingunge afariki Januari 4, 2018.
Kingunge na Peres uzeeni.

Marehemu Kingunge Ngombale Mwiru amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 95 na aliwahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi serikali ikiwa ni pamoja na kuwa waziri asiyekuwa na wizara maalumu, mshauri wa Rais Benjamin Mkapa.

Mbali na nafasi hizo serikalini Marehemu Kingunge ameshika nafasi mbalimbali ndani ya Chama cha Mapinduzi - (CCM) kabla ya kujiondoa ndani ya chama hicho wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
---
Ratiba rasmi ya mazishi ya Mzee Kingunge Ngombale Mwiru (Baba Kinje)

Jumapili tarehe 4/2/2018


- Saa 10:00 jioni mwili kutoka Hospitali kuelekea nyumbani Victoria/Makumbusho Kingunge street, Dar es salaam. 

-Saa 11:00 Jioni mwili kuwasili nyumbani na taratibu za ibada mila na desturi kuendelea usiku mzima(mkesha)
---
Jumatatu tarehe 5/2/2018- Saa 1:00 Asubuhi mpaka saa 2:00 asubuhi waombolezaji kuwasili nyumbani Kwa ajili ya kuanza taratibu za mazishi.

- Saa 2:00 Asubuhi mpaka saa 3:30 asubuhi Kupata kifungua kinywa/Chai Kwa waombolezaji wote

- Saa 4:00 Asubuhi mpaka saa 5:00 misa nyumbani Kwa marehemu

- Saa 6:00 Mchana mwili kuwasili Karimjee hall kwa shughuli ya kuagwa

- Saa 6:00 Mchana 9:00 Alasiri kuaga mwili wa marehemu

- Saa 9:00 Alasiri mpaka 9:30 Alasiri msafara wa kuelekea makaburini Kinondoni

- Saa 9:30 Alasiri mpaka 11:30 Jioni maziko

- Saa 11:30 Jioni 12:30 Jioni kuelekea nyumbani kwa marehemu kwa chakula cha jioni kwa waombolezaji wote

1:30 mpaka 2:45 Usiku chakula cha usiku waombolezaji wote

3:00 Usiku-Hitimisho la shughuli ya Mzee wetu kwa waombolezaji wote.

Tunawashukuru sana waombolezaji wote kwa ushiriki wenu wa Hali na mali katika wakati huu mgumu. Mungu awazidishie.


Bwana ametoa, na bwana ametwaa.


Jina lake na lihimidiwe - AMINA

Imetolewa na:
Omary A. Kimbau
Mwenyekiti wa kamati ya mazishi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: