Tuesday, February 13, 2018

MIC TATA KUKUTANISHA BONGO FLAVA, SINGELI, TAARABU NA HIP HOP JUKWAA MOJA

Uhuru FM kwa kushirikiana na Darlive inakuletea tamasha la Muziki lijulikanalo kama MIC TATA litakalokutanisha miamba ya Muziki hapa nchini litakalofanyika katika ukumbi wa Darlive-Mbagala Zakyeem Februari 24 Mwaka huu.

Mratibu wa show hiyo Said Ambua , amesema Wasanii watakaokutanishwa katika tamasha hilo la MIC TATA ni wa Bongo Flava, Singeli, Taarabu na Hip Hop.

Katika tamasha hilo la Muziki wasanii watakaokuwepo ni Barnaba, Inspector Haroun, Manfongo, Dula Makabila, Joh Makini kutoka Weusi na kwa upande wa taarabu ni Amigo.

Tamasha hilo ambalo kiingilio chake ni shilingi 5,000 litafanyika kuanzia Saa Mbili usiku.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu