Mshindi wa mchezo wa kubahatish wa Tatu Mzuka aitwaye Mrisho Maganga aliyejinyakulia kitita cha shilingi Milioni 22, hivi karibuni amefanikiwa kufanya Dua ya kumshukuru Mungu pamoja na Watoto wa kituo cha Watoto yatima cha Umra Orphanage Center kilichopo Magomeni jijini Dar es Salaam. Maganga alisema kuwa aliamua kufanya Dua pamoja na kula chakula cha pamoja na watoto hao ikiwa ni sehemu ya kumshukuru Mungu kwa kila jambo.Alisema mara baada ya kufanikiwa kuzipata zile fedha ameziingiza kwenye miradi yake aliyokwa ameipanga kuifanya muda mrefu.
Pichani kushoto ni Mwakilishi wa Mchezo wa kubahatisha wa Tatu Mzuka Patronela Nicolaus akiwa pamoja na baadhi ya wadau wa Kituo hicho cha Watoto waishio katika mazingira magumu, Umra Orphanage Center kilichopo Magomeni.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: