Mtoto wa Kitanzania arudishwa nchini baada wazazi wake kuhukumiwa kifo China kwa kukutwa na madawa ya kulevya.

Raia wawili wa Tanzania, Baraka Malali na mkewe Ashura Mussa walikamatwa nchini China Jan. 19 mwaka huu kwenye uwanja wa ndege wa Baiyun Guangzhou, wakiwa wamemeza tumboni dawa za kulevya, walihifadhiwa kwenye chumba maalum kwa muda Baraka alitoa pipi 47 kwa njia ya haja ambapo mkewe alitoa pipi 82.

Watuhumiwa hao walikatwa wakiwa wameandama na mtoto wao mwenye umri wa miaka 2 na miezi 9. Serikali ya China iliwasiliana na serikali ya Tanzania kuhusiana na suala la mtoto huyo ambapo walikubaliana kumrudisha mtoto huyo nchini, mtoto huyo aliingia nchini jana majira ya saa saba mchana akiwa ameambatana na Afisa wa wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kikanda.

Serikali kupitia Mamlaka ya kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya na Ustawi wa Jamii inafanya jitihada za kuwasiliana na ndugu na jamaa wa watuhumiwa ili kuhakikisha mtoto huyo anakabidhiwa kwao kwa jaili ya malezi na matunzo.

Taarifa Na: Rogers W. Siyanga
Kamishna Jenerali:
Mamlaka Ya Kudhibiti Na Kupambana Na Dawa Za Kulevya Nchini.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: