Na Amini Mgeni.

William Franklin Graham Jr. Maarufu Billy Graham moja ya wahubiri maarufu zaidi duniani amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 99,Billy ni miongoni mwa wakristo wa pekee dunia anastahili kuitwa mwamba na jabali la injili duniani ama jina lolote la kutukuka ambalo unaweza tumia naama anastahili,,

Billy Graham alizaliwa November 7 mwaka 1918 ana amefariki leo February 21, 2018 na alikuwa mkirsto wa dhehebu la Baptist,na amehubiri mikutano na nje na ndani kwa zaidi ya miaka 60 tangu mwanzoni mwa miaka ya 1940 na aliacha kufanya mikutano yake mwaka 2005 baad aya umri kusonga

Billy Graham umebeba upekee kwani alikuwa ni mshauri na baba wa kiroho wa kiroho wa marais wote wa Marekani kwa muda mwingi tangu miaka ya 1960 kuanzia kwa Rais Harry Truman hadi Barack Obama takwimu zinaonesha kuwa Billy Graham amehubiri injili kwa wanadamu zaidi ya milioni 215 katika mataifa zaidi ya 185 duniani.

Upekee wa Billy Graham alishiriki katika vita ya ubaguzi wa rangi nchini Marekani waziwazi na alikuwa rafiki wa karibu sana wa Martin Luther King jr na alikwenda kumtoa jela mwaka 1960 baada ya Martin Luther kushikilia kwa kuandaa maandamano.

Billy Graham amemaliza mwendo akitajwa kuwa binadamu aliyehubiri injili kwa muda mrefu zaidi katika historia ya dunia.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: