Ajali mbaya imetokea jana usiku huu Mandela road maeneo ya TOT kabla hujafika traffic light za Tabata... Mwandishi wa gazeti la uhuru, Mariam Mziwanda anusurika kifo katika ajali mbaya iliyotokea majira ya saa 4:40 usiku (Februari 22, 2018) katika maeneo ya TOT- Tabata Jijini Dar es Salaam baada ya gari lenye namba za usajiri T222 DJX alilokuwa akiendesha kufinywa na magari mawili na kukandamizwa na kontena.

Wakizungumza na Azam TV dakika chache baada ya ajali, baadhi ya shuhuda na wasamalia wema waliomsaidia Mariam kutoka katika gari lake kupitia kioo cha nyuma wanasema chanzo cha ajali hiyo ni daladala iliyokuwa ikijaribu kuhama upande wake na kuingia upande wa pili.

Akiwa katika hali ya tahamaki, huku akilia kwa kwikwi, Mariam alisikika akimshukuru Mungu kwa kumuokoa katika ajali hiyo. “Asante Mungu nimepona… nimepona jamani…nisaidieni jamani kuongea na ndugu zangu.” Azam TV ilijaribu kuwasiliana na mumewe, lakini namba yake ilikuwa ikiita bila majibu.

Mariam ambaye ni majeruhi pekee alikimbizwa hospitali ya Muhimbili na Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Said Kubenea. Mariam amepata majeraha maeneo ya miguu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: