Mshindi wa Promosheni ya SMATIKA na Intanenti Esha Nasir akitoa shukurani kwa kampuni hiyo kwa kushinda modern ya maajabu ambayo ameamua kumzawadia mtoto wake leo katika makao makuu ya Airtel Jijini Dar es Salaam.
 Mtoto Arif Nasir aliyezawadiwa Modern ya Maajabu na mama yake akizungumza kuwa ataitumia vema Modern hiyo kwa matumizi ya mafunzo ya shuleni leo katika makao makuu ya Airtel Jijini Dar es Salaam.
Kulia Meneja Miradi Airtel Tanzania Jane Matinde akimkabidhi Mshindi wa Promosheni ya SMATIKA na Intanenti Isack John Simu aina ya Smartphone leo katika makao makuu ya Airtel Jijini Dar es Salaam.

Picha/Habari: Cathbert Kajuna-Kajunason/MMG.

KAMPUNI ya Simu za mkononi Airtel Tanzania imendelea kutoa donge nono kila siku kwa wateja wake kupitia Promosheni ya SMATIKA na Intanenti.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam mara baada ya kutoa zawadi kwa washindi hao Meneja Miradi Airtel Tanzania Jane Matinde, amesema promosheni hiyo ya SMATIKA na Intanenti inayoendelea kufanyika ambapo kila siku wateja 10000 kujishindia GB1 kwa wateja wake.

Aidha washindi hao 2 waliokabidhiwa zawadi zao ni Isack John aliyejishindia simu aina ya Smartphone, pamoja na Esha Nasir aliyejishindia Modern ya maajabu inayounganisha watu 20 ambayo ameamua kumzawadia mtoto wake Arif Nasir kwa ajili ya matumizi ya mafunzo ya shuleni

"Huwa najiunga muda wa maongezi pamoja na bando la intanenti mpaka imenifanya kuibuka mshindi, nimejishindi simu aina ya Smartphone, "amesema Mshindi Isack John.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: