Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati akielezea maandalizi kabambe ya Tamasha la pasaka linalotarajia kufanyika Aprili mosi katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza na baadae tamasha hilo April 2, 2018 tamasha hilo litafanyika katika uwanja wa Halmashauri ndani ya Bariadi mkoani Simiyu.
Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati akielezea maandalizi kabambe ya Tamasha la pasaka linalotarajia kufanyika Aprili mosi katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza na baadae tamasha hilo April 2,2018 tamasha hilo litafanyika katika uwanja wa Halmashauri ndani ya Bariadi mkoani Simiyu.

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Mwimbaji Mahiri wa nyimbo za Kiroho (Injili) Rose Muhando anatarajia kuizindua albamu yake ndani ya Tamasha la Pasaka linalotarajiwa kufanyika kufanyika Aprili mosi katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza na baadae tamasha hilo April 2,2018 litafanyika katika uwanja
wa Halmashauri ndani ya Bariadi mkoani Simiyu .

Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama ambao ndiyo waandaaji wa tamasha hilo, amesema maandalizi ya tamasha hilo yanaendelea vizuri na wanatarajia kuanzia katika jiji La Mwanza ndani ya Uwanja wa CCM-Kiruma Aprili 1, 2018 na kuelekea uwanja wa Halmashauri mjini Simiyu.

"Kwa kipindi kirefu Mwimbaji Rose Muhando amekuwa kimya kwa muda mrefu ila kwasasa namtangaza Kinara Rose Muhando ndiyo atakayeongoza jahazi la Tamasha la Pasaka kwa Mwaka 2018 hivyo wananchi mjitokeze kwa Wingi," amesema Msama.

Aliongeza kuwa mbali na uzinduzi huo, tukio lingine kubwa litakalofanyika ni kuombea nchi amani,hukua kauli mbiu itakuwa "Upendo na Amani"

"Nipende kuwaomba wananchi wajitokeze kwa wingi katika tamasha la Pasaka ambalo litakuwa la namna yake na waje wajionee vipaji lukuki kutoka ndani ya Tanzania na nje.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: