Na Mwandishi wetu,

WAZIRI mwandamizi mstaafu wa serikali ya awamu ya nne, pamoja na wapambe wake waliokuwa wananufaika na manunuzi ya kimataifa yanayohusisha miradi mikubwa hapa nchini, wameanza mikakati ya kumchafua Rais Dk. John Magufuli.

Taarifa inaeleza watu hao bila kujali kama wanalikuwa wanaiingizia hasara Taifa kutokana na ushiriki wao wa kuleta kampuni za kimataifa na kuhakikisha zinapata zabuni mbalimbali zilizotangazwa na Serikali na hatimaye kugawana fedha na kuzitumia kwa matumizi yao binafsi.

Watu hao, wanaelezwa kukasirishwa na kitendo cha Rais Dk. Magufuli kuzuia njama zilizowekwa kuliibia taifa zaidi ya sh. bilioni 400 katika mradi wa uhamiaji wa kimtandao maarufu kama E-migration unaojumuisha vipengele vya E-Passport, E-Visa, E- Border na nyinginezo

Taarifa za uhakika ambazo gazeti hili imezipata kutoka kwa watu wa karibu wa Waziri huyo anayejiandaa kugombea Urais kupitia CCM katika kura za maoni uchaguzi ujao na hatimaye kuhamia Upinzani ikiwa hatafanikiwa kumshinda Rais Dk. Magufuli katika kura za maoni za ndani ya Chama hicho.

Gazeti hili, limebaini kiongozi huyo, ameanzisha kelele zinazopigwa na gazeti moja la kila wiki kuhusiana na kunyimwa zabuni kwa kampuni ya DeRaLue ya Uingereza zinatokana na Waziri huyo kuwa kuwaahidi mambo makubwa wabia wa kampuni hiyo kutokana na ushawishi wake wa serikali iliyopita kama alivyofanikiwa kwenye miradi mbalimbali ukiwemo ule wa Vitambulisho vya Taifa unaosimamiwa na NIDA kwa kumtumia mmoja wa watu mashuhuri hapa nchini anayejitambulisha kama jasusi (jina linahifadhiwa).

Mchakato wa mradi wa E-Migration unasemwa kuwa ulianza mwaka 2013 wakati Waziri huyo akiwa ni miongoni mwa mawaziri wenye ushawishi mkubwa na kwamba ni yeye aliyewafuata Waingereza hao na kuwakaribisha waje kuwekeza kwenye mradi huo.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa alikuwa ana uhakika kuwa katika utekelezaji wa mradi huo, tayari yeye angekuwa ndiye Rais wa awamu ya tano kwa matarajio yake ya kushinda uchaguzi wa mwaka 2015 jambo ambalo halikutokea kama alivyotarajia.

Taarifa zinasema kampuni hiyo ni miongoni mwa makampuni ya kimataifa yaliyomchangia kiasi kikubwa cha fedha alichokitumia kufanikisha kampeni zake za ndani ya Chama chake za kugombea kupendekezwa kuwa mgombea Rais ambapo vyanzo vingine vya fedha za kampeni alizozitumia zinatajwa kuwa ni mradi wa vitambulisho vya taifa na fedha za Libya maarufu kama fedha za Gaddafi zaidi ya dola milioni 21 za kimarekani.

Kushindikana kukamilika kwa mradi huo kabla ya mwaka 2015 inasemekana kuwa ilikuwa ni neema kwa watanzania kwani imewasaidia kuokoa zaidi ya bilioni 400 ambazo zingetokana na gharama za ziada kuufanikisha mradi kwani Rais Magufuli alivyofahamishwa kuhusu madudu hayo aliagiza mchakato huo ufanyike kwa watu wenye ueledi na wanaozingatia ubora wa kimataifa huku gharama zao zikiwa nafuu na zenye tija.

Kampuni inayopigiwa debe na Waziri huyo inasemwa kuwa haikuwa tayari kutengeneza hati za kusafiria kutumia material ya ‘Polycarbonate’ huku yakiwa na ‘Chip’ ya mawasiliano ndani yake na badala yake ilitaka kutumia karatasi za kawaida kama za kuchapia gazeti kitu ambacho ni kinyume na makubaliano ambayo yalitajwa kuingiwa.

Aidha kampuni hiyo ilidai kuwa ingefunga mfumo huo katika mikoa nane tu kati ya mikoa 31 ya Tanzania na kwamba kila mkoa mmoja wa nyongeza ambao serikali ingetaka kufunga mfumo huo ilitakiwa kulipa Paundi laki moja za kiingereza sawa na zaidi ya milioni 314 za kitanzania

Taarifa zaidi zinasema kuwa ikiwa Tanzania ingetaka kufunga mfumo katika mikoa yoye ingelazimika kulipa gharama za zaidi sh. bilioni 7.1 nje ya mkataba na kwa kila huduma inayoongezeka ingelipiwa sh. milioni 314 jambo ambalo linafananishwa na mkataba tata wa Richmond

Jamvi la Habari linaweza kuthibitisha kuwa kampuni hiyo ilitaka kulipwa kiasi cha sh. bilioni 13.7 za kitanzania kwa ajili tu ya kuufunga mfumo huo katika jumla ya balozi 44 duniani fedha ambazo ni ziada ya makubaliano

Vile vile wajanja hao waliakataa kuufunga nchini mfumo wa kutunza kumbukumbu za taarifa za siri za Passpoti (Servers) hizo na badala yake kuufunga nchini Uingereza ili waweze kudhibiti mfumo mzima wa usafiri wa kimataifa wa watanzania wote wakiwemo viongozi jambo ambalo linasemwa kuwa ni hatari kwa usalama na ulinzi wa taifa la Tanzania

Taarifa zaidi zinaeleza mambo mazito yameibuka yakilihusisha gazeti moja la kila wiki kuhongwa mamilioni ya fedha ili kuichafua serikali wakiituhumu kwa tuhuma za uongo kuhusiana na mradi wa hati za kusafiria na uhamiaji kwa ujumla.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: