Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Lilian Liundi akitoa ufafanuzi wa jambo fulani mapema leo jijini Dar es salaam katika mkutano na waandishi kuhusu kongamano la Wanawake Uongozi.

Waandishi wa habari wakiendelea na kazi yao.

NA VICENT MACHA - DAR ES SALAAM.

SERIKALI imetakiwa kuzitambua kazi za kutoa huduma zinazotekelezwa na wanawake na kuziingiza katika Mipango ya Taifa kwani zinaweza kusaidia kuongeza pato la Taifa.

Hayo yamesemwa mapema leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia (TGNP) Bi. Lilian Liundi alipokuwa akitoa Mhuktasari wa Kongamano la Wanawake na Uongozi.

Kongamano hilo linatarajiwa kufanyika siku ya jumanne ya tarehe 27 Mlimani City jijini Dar es salaam, likihudhuliwa wanawake mbalimbali walio katika nafasi za uongozi na waliostafu.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa kuna haja ya serikali kuzitambua shughuli mbalimbali zinazotolewa na wanawake kama huduma kwa lengo la kujipatia kipato kwani uchunguzi umebaini kuwa wanawake hutumia muda wa masaa 10 mpaka 15 kwa siku kwa shughuli hizo hivyo wanakosa muda wa kufanya shughuli za kujipatia kipato.

Aidha Mkurugenzi huyo aliendelea kusema kuwa lengo kuu la Kongamano hilo ni wanawake kwa pamoja kuweza kujadili namna gani wataweza kuongeza nafasi za uongozi na maamuzi kwani bado hawajaweza kufikia lengo ambalo ni 50 kwa 50.

Lakini pia kuweza kusherekea, kupongezana na kuajadili changamoto mbalimbali anazokutana nazo mwanamke katika Nyanja ya elimu, afya na umiliki wa ardhi swala ambalo bado ni changamoto kubwa kwa wanawake wengi hivi sasa.

Bi. Lilian aliendelea kusema kuwa kutakuwa na kuenzi na kukumbuka mchango uliotolewa na wanawake ambao walikuwa katika ngazi za uongozi maamuzi kuanzia ngazi ya jamii mpaka taifa.

Mgeni Rasmi katika Kongamano hilo anatarajiwa kuwa Waziri msataafu Mama Marry Nagu, lakini pia kutakuwa na wadau zaidi ya 250 wanawake kwa wanaume viongozi wa sasa na wastaafu katika kuhakikisha kongamano hilo linaleta tija kwa jamii yetu

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: