Wafanyakazi wa TBL wakipata mafunzo sambamba na burudani za vinywaji baada ya saa za kazi.
Wafanyakazi wa TBL Mwanza wakifuatilia mafunzo ya mahusiano na afya.
Wafanyakazi wa TBL Arusha wakifutilia mafunzo.
TBL Moshi hawakubaki nyuma katika mafunzo hayo.
TBL Mbeya nao walishiriki mafunzo na mijadala ya mahusiano

Kampuni ya TBL Group chini ya kampuni mama ya ABInBev, imeitumia Siku ya Wapendanao kuandaa semina za wafanyakazi wake kuhusiana na masuala ya mahusiano katika familia, zilizoendeshwa na wataalamu wa masuala ya Saikolojia na ushauri nasaha kutoka taasisi mbalimbali za mafunzo nchini. Semina hizo zilifanyika katika viwanda vyake vilivyopo katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya, Kilimanjaro na Arusha.

Kwa kutumia kauli mbiu ya ‘Nogesha Upendo Valentine hii’ wafanyakazi walipata fursa ya kupata mafunzo,na kushiriki mijadala kuhusiana na mahusiano bora katika ndoa na familia sambamba na changamoto mbalimbali zilizopo, pia waliweza kupata majibu na ushauri wa changamoto hizo waliokuwa wakiendesha mafunzo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: