Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora akiongea na wafanyakazi wa kiwanda cha Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, (katikati) Kaimu Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Bw. John Kaswalala, jijini Dar es Salaam tarehe 20 Februari 2018.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora akifurahia kazi nzuri inayofanywa na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali alipofanya ziara fupi kiwandani hapo jijini Dar es Salaam tarehe 20 Februari 2018.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora akishauri jambo kwa wataalamu wa kiwanda cha Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali akikagua mitambo alipofanya ziara katika kiwanda hicho jijini Dar es Salaam tarehe 20 Februari 2018.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Kaimu Mpiga Chapa Mkuu wa Serika alipotembelea kiwanda hicho na kukutana na wafanyakazi jijini Dar es Salaam tarehe 20 Februari 2018.
---
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora awataka watumishi wa ofisi ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali kujituma na wawe wabunifu ili kuzalisha kwa ufanisi zaidi.

Amesema hayo alipotembelea kiwanda cha Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali kilichopo jijini Dar es salaam,tarehe 20 Februari 2018.

Amewasisitiza wafanyekazi kwa nguvu, wajue vifaa wanavyotumia na kuvielewa ili kuweza kufanya kazi kwa urahisi na kuepuka uharibifu wa mashine hizo, watambue kuwa Serikali inazidi kuboresha mazingira ya kazi na taratibu za kuendesha shuguli zake za kiuchumi.

“Tunaishi katika ulimwengu wa maarifa,hivyo maarifa tuyatumie kazini kwa kuwa wabunifu na kufahamu vizuri mitambo na vifaa tunavyotumia ili tuweze kuzalisha kwa ufanisi ili wote tufaidike na matunda ya uzalishaji huo.” Alisema Prof. Kamuzora.

Akielezea juu ya uendeshaji shughuli za kiwanda hicho Kaimu Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Bw. John Kaswalala alisema, kiwanda hicho kinaendelea kukua kiuchumi na kuimarika. Aidha, watumishi wa Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali wamempongeza sana Prof. Kamuzora kwa utendaji wake na kufika kwake katika ofisi zao, na kuomba serikali izidi kuwawezesha kwa vifaa, mitambo na teknolojia ili wazidi kuzalisha zaidi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: