Na Humphrey Shao, Globu Ya jamii

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage anataraji kufungua kongamano kuhusu Maendeleo ya Viwanda Tanzania litakalo fanyika katika chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere February 23 Mwaka huu.

Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo Afisa Habari wa chuo Hicho

Evelyn Mpasha amesema kuwa Kongamano hilo kubwa litawaleta karibu wadau mbalimbali wa masuala ya maendeleo ya Viwanda nchini.

“Kongamano hili litaangazia Masuala ya Maendeleo ya Uchumi , Uwekezaji Endelevu katika Viwanda, Ujasiliamali katika Uwekezaji katika Viwanda kwa mfumo wa ushirikiano kati ya sekta ya Umma na sekta binafsi” amesema Mpasha.

Kwa upoande mmoja wa watoa mada katika kongamano hilo Binto Mawazo amesema kongamano hili ni sehemu ya juhudi za chuo kushiriki katika kuunga mkono juhudi za serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuipeleka Tanzania katika uchumi wa Viwanda .

Binto amesema kuwa MNMA kama chuo ni wadau Muhimu sana katika kukiwezesha wananchi kufika malengo ya Rais kuipeleka nchi katika uchumi wa kati.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: