Mwalimu Daudi Kyeya Mwalimu Mkuu Shule ya msingi Kajunguti iliyopo Wilayani Missenyi akimuonyesha Balozi Dkt. Kamala Mbunge wa jimbo la Nkenge mazingira ya shule hiyo inayokabiliwa na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na uhaba wa vyumba vya madarasa na vyoo vya Walimu

Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dkt. Kamala ametembelea shule hiyo mapema ya leo March 6, 2018 kwa lengo la kuongea na Walimu ili kubaini sababu za Ufaulu hafifu kwa ujumla shuleni hapo hapo pia amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Missenyi kutembelea Shule hiyo na kubainisha mikakati ya muda mfupi na mrefu ya kupata ufumbuzi wa changamoto zinazokakabili Shule hiyo. 

Aidha Balozi Kamala amehaidi kukutana na Wadau wengine wa Shule hiyo kwa nia ya kutafuta ufumbuzi wa matatizo. 

Wadau wengine ni Halmashauri ya Wilayaya Missenyi, Serikali Kuu, Jamii, Serikali za Vijiji vya Bulembo na Mushasha, Uongozi wa ELCT Dayosisi ya Kanda ya Kaskazini Magharibi ambayo awali ndio waliotoa majengo ya shule hiyo mwaka 1994 kuhudumia watoto wa wafanyakazi waliokuwa wameajiliwa katika miradi mbalimbali ya ELCT katika maeneo hayo.
Wanafunzi wa darasa la tatu na darasa la awali wanasomea katika madarasa ya Udongo na huku walimu wakitumia choo cha Nyasi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: