Meneja Mkuu wa EFM Radio, Dennis Busulwa (SEBO), Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam leo juu ya shamrashamra za Efm Kutimiza miaka minne sanjari na uzinduzi wa Shindano la Shika ndinga linaloendeshwa na kituo hicho cha Radio kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
 Afisa Uhusiano wa Shirika la Simu nchini(TTCL), Nicodemus Mushi akizungumza na Waandishi wa habari juu ya udhamini wa shirika lake katika mashindano ya shika ndinga kote nchini.
 Afisa Habari wa Kampuni ya Michezo ya Kubahatisha ya Tatu Mzuka ,Petronila Mtatiro akieleza namana watu watakavyoweza kujishindia zawadi mbalimbali wakati wa shindano la shika ndinga.
 Mkurugenzi wa kampuni ya Chotec Limited inayosambaza vilainishi vya Shell, Tanzania, Choba Mumba akieleza namna wao watakavyoweza kusambaza vilainishi maalum vya pikipiki nchini.
 Meneja Matukio wa Kampuni ya Efm Radio, Jesca Mwanyika akizungumza juu ya matokeo ya washindi wa shindano la Shika ndinga katika msimu uliopita .
 Baadhi ya Wadau na wadhamini wakifatilia mkutano wa Waandishi wa habari juu ya shindano la Shika Ndinga na Miaka Minne ya Efm.
Sehemu ya Waandishi wa Habari wa waliohiriki Mkutano juu ya shindano la shika ndinga na Miaka minne ya Efm.

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.

Mkurugenzi Mkuu wa kituo cha Efm Radio, Dennis Busulwa(SEBO) amesema kampuni yake imewekeza kiasi cha zaidi Milioni 300 kwa ajili ya shindano lake la Shika Ndinga litakalofanyika katika mikoa 6 ya Tanzania bara na kuanza kutimua vumbi Dar es Salaam katika uwanja wa Mwembe Yanga.

Sebo amesema hayo jijini Dar es Salaam leo alipokuwa anazungumza na Waandishi wa habari juu ya uzinduzi wa shindano hilo na maadhimisho ya miaka minne ya Efm Radio na kuongezeka kwa masafa kwa kutoka mikoa sita hadi kufika kumi.

"Efm Radio imekuwa na bidhaa mbalimbali za uwezeshaji kwa wasikilizaji wake ambapo shika ndinga kwa mwaka huu 2018 linaweza kuwafikia watanzania katika mikoa sita zaidi ikiwa ni lengo la uwezeshaji katika jamii "amesema Sebo.

Amesema Shindano la shika ndinga mwaka huu linatarajia kufanyika kwa wiki 7 katika mikoa sita amabayo ni Dar es Salaam, Tanga, Mwanza, Mtwara , Mbeya na Pwani ambapo litaanza tarehe 7 April hadi mei 15 ikihusisha jumala ya Pikipiki 14 na gari aina ya kirikuu mbili.

katika hatua nyingine Sebo alitumia mkutano kuwaeleza waandishi wa habari juu ya mafanikio ya Radio yao katika miaka minne tangu kuanzishwa kwake kwa kuwa radio namba moja kwa kusikilizwa kwa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani huku ikiwa namba mbili katika mikoa ya bara.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: