Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Finca MicrofinaceTanzania , Issa Ngwegwe akizungumza na waandishi wa habari kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka ya 20 ya Taasisi hiyo jijini Dar Es Salaam leo. Pembeni ni Mwenyekiti wa bodi ya Finca, Mike Gama-Lobo na Rais na Afisa mtendaji mkuu wa Makampuni ya Finca Duniani, Andree Simon.
 Rais na Afisa mtendaji mkuu wa Makampuni ya Finca Duniani, Andree Simon akizungumza na waandishi wa habari kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka ya 20 ya Taasisi hiyo jijini Dar Es Salaam leo.
Mwenyekiti wa bodi ya Finca, Mike Gama-Lobo akizungumza na waandishi wa habari kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka ya 20 ya Taasisi hiyo jijini Dar Es Salaam leo.
 Meza kuu.

Na Mwandishi Wetu.

Benki ya FINCA Microfinance, moja kati ya benki maarufu zinazotoa mikopo midogo midogo nchini Tanzania, imefikisha miaka 20 tangu ianzishwe Tanzania.

Sherehe zinatarajiwa kuanza kwa hafla ya kupendeza na chakula cha jioni itakayokuwa imepambwa kwa rangi nzuri katika hoteli ya Serena Jijini Dar Es Salaam.

FINCA imesisitizia nia yake ya kuendelea kuwa taasisi inayoongoza katika ushirikishaji wa kifedha nchini.

Sherehe hizo zinatarajiwa kuhudhuriwa na zaidi ya wageni 300 ambao ni pamoja na Bodi ya Wakurugenzi wa FINCA, Uongozi wa FINCA, wafanyakazi na viongozi wa juu kutoka katika mtandao wa FINCA Duniani.

Raisi na Mkurugenzi Mtendaji wa FINCA Microfinance Holding Company, Andree Simon aliipongeza FINCA Tanzania kwa safari yake yenye mafanikio waliopata ambayo imewafikisha katika miaka 20 ya maendeleo na mabadiliko, yaliyosaidia taasisi hiyo kuendelea kuwa taasisi ya kutoa mikopo midogo na kufikia kuwa Benki ya kutoa mikopo midogo ilivyo sasa.

Makamu wa Raisi wa Tanzania Mheshimiwa Samia Sululu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya chakula cha jioni kwa kusherehekea miaka 20 ya Benki hiyo.

Mwenyekiti wa Bodi ya FINCA ambaye pia ni Makamu wa Raisi na Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika Mike Gama-Lobo aliwashukuru wajumbe wenzake wa Bodi na viongozi wa juu wa Benki kwa kuonyesha juhudi za kuigwa ambazo zimepelekea katika kukua kwa FINCA, kufikia maendeleo makubwa katika mazingira ya biashara yenye changamoto nyingi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya FINCA Microfinance, Tanzania Issa Ngwegwe amesema: "Mafanikio haya ya miaka 20 ni ushuhuda wa hamasa ya FINCA katika kutoa huduma za kifedha zilizokuwa salama na kuwawezesha wajasiriamali wadogo nchini Tanzania

Akielezea kuhusu hali ya ukopeshaji ya FINCA, Ngwegwe alisema: "Tangu FINCA ilipoanzishwa mwaka 1998, tumeweza kutoa zaidi ya TZS 900 Billioni katika mikopo kwa wajeja zaidi ya milioni 1.1 wakiwemo wajasiriamali wadogo, kukuza biashara zao, kutengeneza ajira na kuboresha kiwango cha maisha. Katika miaka ijayo, tutaendelea kutekeleza wajibu wetu katika kuboresha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wafanyabiashara wadogo (SMEs) ambao ndio msingi wa maendeleo ya uchumi wa nchi yetu.

Aliongeza kusema zaidi kwamba FINCA ilikuwa imejidhatiti katika mpango wake wa kuondoa umaskini kupitia suluhisho la kudumu ambalo linasaidia watu kujenga rasilimali zao, kutengeneza ajira na kuboresha kiwango chao cha maisha.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: